Tarehe 22 Jamadil Ula kumbukumbu ya kufariki kwa mtu mwenye karama ndugu wa imamu Ridha na baba mdogo wa imamu Jawaad (a.s)..

Malalo ya Qassim bun Mussa Alkaadhim (a.s)
Ukitaka uhai wenye maisha mazuri, nenda kazuru malalo ya Qassim.

Katika malalo hayo matatizo hutatuka, sawa na nyumba inavyo tembelewa na watu wengi.

Na kukutatulia matatizo yaliyo shindikana, na kukuondoshea ubaya unao kushambulia.

Siku ya 22 Jamadil Ula ni siku yenye machungu makubwa kwa waislamu na hasa wafuasi wa Ahlulbait (a.s), ni siku ya kukumbuka kufariki kwa mtu aliye kua na karama nyingi Qassim bun imamu Mussa Alkaadhim (a.s) alikua mtu mwenye heshima kubwa mtakasifu anatokana na kizazi cha mtume (s.a.w.w) alipambika na sifa za uimamu, alikua mtu wa pekee katika zama zake, kutokana na uchamungu na unyenyekevu alio kua nao, alipata matatizo makubwa katika mji wa Madina baada ya kuondoka ndugu yake imamu Ridha (a.s).

Hali ya Qassim (a.s) ni sawa na hali ya watu wengine wa nyumba ya mtume watakasifu, alilazimika kuhama katika mji wa babu yake (Madina) na kuelekea Iraq, alifatana na msafara wa biashara ambao aliachana nao walipo fika katika mji wa Kufa, alibanywa sana na kufanyiwa maudhi mengi kwa sababu alikua anaheshimika na kukubalika sawa na ndugu yake imamu Ridha (a.s), kutokana na uadui waliokua wakifanyiwa watu wa nyumba ya mtume (a.s), maimamu walitumia siasa ya kumtanguliza mbele za watu mtoto ambaye sio maasumu anaye fanana na maasumu kielimu na uchamungu ili kumlinda yule maasumu, pia kuna siri ya Mwenyezi Mungu katika swala hilo, watoto wa imamu Mussa Alkaadhim (a.s) pia ilikua hivyo, walienea sehemu mbalimbali, na aliye pata umashuhuri mkubwa alikua ni Qassim (a.s) ambaye alijulikana kwa ukubwa wa elimu, umakini wa akili, na uchamungu.

Alikua ni mtukufu sana, yatosha katika kuelezea utukufu wake riwaya iliyo pokelewa na thiqatul islamu Shekh Kuleini katika kitabu cha Kaafi katika mlango wa maelezo kuhusu imamu Ali bun Mussa (a.s) kutoka kwa Yazid bun Sulait kutoka kwa imamu Alkaadhim (a.s) walipo kua njiani kuelekea Maka imamu (a.s) alimuambia kua: (…Nakuambia ewe baba Ammaara mimi nilipo toka nyumbani nimemuhusia mwanangu fulani na kumshirikisha mwanangu katika dhahiri na kumuhusia katika siri nikamtenga pekeyake, lau kama jambo lingekua kwangu ningempa (uimamu) mwanangu Qassim kutokana na mapenzi yangu kwake, lakini jambo hili lipo kwa Mwenyezi Mungu mtukufu anamteua amtakaye…).

Kuna riwaya nyingine kutoka kwa Shekh Kuleini, imepokewa na Suleiman Jafari anasema: Nilimuona Abuul hassan (a.s) alipo karibia kufariki mmoja wa watoto wake alimuambia mwanae Qassim: (Simama ewe mwanangu na usomee kichwani kwa ndugu yako (Waswaafaati swafaa hadi mwisho) akasoma, alipofika: (..Ahum ashadu khalkan am mankhalakna..) yule ndugu yake akafariki).

Qassim (a.s) alifariki baada ya kuugua sana katika kitongoji cha Suriy mtaa wa Bakhamra, malalo yake matakatifu yamejengwa hapo na sasa hivu kuna kubba la dhahabu na minara mizuri, naru ya utukufu wake na karama zake zinaendelea hadi leo, ndimi zinashindwa kuelezea wingi wa karama zake, na wenye kusifu hawawezi kumaliza sifa zake hakika amekaa katika nyoyo za watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: