Kufatia kumalizika kwa likozo za shule, nayo idara ya makuzi ya watoto chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekhitimisha ratiba ya hema za Scout, ambayo ilifanyika kwa lengo la kuendeleza vipaji vya wanafunzi kielimu, kimichezo na kuhakikisha wanatumia vizuri kipindi cha likizo, hema hizo ambazo zilihusisha wanafunzi wa rika zote ziliwekwa katika jengo la Shekh Kuleini (q.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya katika barabara ya Bagdad/Karbala.
Kiongozi wa idara ya usimamizi wa hema hizo aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kufatia kumalizika kwa kipindi cha likizo, tunahitimisha ratiba ya hema za Scout tuliyo ifanya kwa wanafunzi wa rika zote, hema la kwanza lilikua la wanafunzi wa upili (sekondari) (Sayyidul Maau) miongoni mwa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s), halafu kulikua na hema la (Jabali ya subira) hema hili lilidumu siku tatu na walishiriki wanafunzi (80), lililenga kuongeza uwezo wa wanafunzi kielimu na kimuili (mazoezi) pamoja na kugundua vipaji vya wanafunzi katika usomaji wa Qur’an, uchoraji, maigizo, hati na mengineyo, tuliweka ratiba maalumu ya kugungua vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza pia kulikua na ratiba ya utoaji wa mihadhara na utoaji wa huduma ya kwanza, katika vipindi vya utoaji wa mihadhara ya kidini tulishirikiana na kitengo cha dini cha Ataba tukufu”.
Akaendelea kusema kua: “Hema la pili lilihusu wanafunzi wa shule za msingi, na walishiriki zaidi ya wanafunzi (80) lilipewa jina la (Nuru za Fatuma) na lilijikita katika mapumziko (picnic), usomaji wa Qur’an, Kaswida na Historia za maasumina (a.s) pamoja na kwenda katika mji wa Sayyid Auswiyaau uliopo katika barabara ya Bagdad/Karbala kwa ajili ya mapumziko na kupata mafundisho mbalimbali, pia kulikua na hema lililo jumuisha wanafunzi wa O levo na A levo nalo lilidumu siku tatu, lilikua linaitwa hema la (Fadak Zaharaa) washiriki walikua zaidi ya mia moja lilijikita katika mazoezi na utoaji wa mihadhara kuhusu maendeleo ya mwanadamu na huduma za uokozi, hema hili lilikua tofauti na mengine kwa sababu shuguli zake zilikua za ndani na wanafunzi walilala ndani ya hema”.
Akaendelea kufafanua kua: “Hema la mwisho lilikua linaitwa (Watumishi wa Zaharaa) lililo andaliwa kwa ajili ya wanajumuia wa Scout ya Alkafeel, na lilijikita katika utoaji wa semina ya kujenga uwezo, lilidumu kwa siku nne na walishiriki zaidi wa wanajumuia ishirini, ilitolewa mihadhara mbalimbali na mambo mengine mengi ya kuwajengea uwezo, mwisho wa ratiba hizi vilitolewa vyeti vya ushiriki kwa washiriki wote pamoja na zawadi kwa wale waliofaulu katika mashindano mbalimbali yaliyo tolewa wakati wa ratiba wa hema hizo”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaandaa na kusimamia ratiba nyingi za kielimu na kitamaduni ndani na nje ya Ataba tukufu, miongoni mwake ni hema za Scout kwa wanafunzi ambazo zina mchango mkubwa katika kulea na kukuza vipaji vya wanafunzi na kuhakikisha wanafahamu misingi ya uislamu kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya mtume na Ahlulbait zake (a.s) na kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yao kwa mustakbali boro wa maisha yao.