Ugeni wa Ataba tukufu ukiongozwa na muheshimiwa Sayyid Swafi (d.i) wahudhuria hafla ya kuwakumbuka mashahidi wa kikosi cha tisa..

Maoni katika picha
Ugeni wa heshima ukiongozwa na kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na katibu mkuu na naibu wake wakiwa na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati ya uongozi na wakuu wa vitengo pamoja na baadhi ya watumishi, wamehudhuria hafla ya kuwakumbuka mashahidi kumu wa kikosi cha tisa cha hashdi sha’abi katika Munadhamat Badri ambao waliuawa hivi karibuni katika eneo la Daur ndani ya mji wa Tikriti kutokana na shambulio la magaidi ya kidaesh.

Mashahidi hao kumi: nane kati yao ni wakazi wa mji wa Karbala tukufu na wawili wakazi wa Daur, waliuawa tarehe 17/02/2017m.

Hafla ya taazia imefanyika katika mji wa Karbala tukufu katika kitongoji cha Huru Riyahi (r.a) ndani ya jengo la Jaamiu Imamu Ali Alhaad (a.s), ilipata mahudhurio makubwa kutoka kwa familia za mashahidi na wakazi wa Karbala pamoja na wapiganaji wa hashdi sha’abi.

Muheshimiwa Sayyid Swafi na ugeni aliofatana nao walitoa mkono wa pole kwa familia za mashahidi watukufu, na wakasema kua hakika damu hii iliyo mwagika ndio itakayo ikomboa Iraq kutoka kwa magaidi na kuirejesha haki kwa watu wake, na hizi ni bishara za ushindi, akasisitiza kua; Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu mtukufu anaendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa kuzisaidia familia za mashahidi na majeruhi kutokana na utukufu mkubwa walio nao kwa wairaq wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: