Idara ya ushonaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza kifaa cha kudarizi cha kisasa chenye vichwa nane kinacho tumia tanakilishi (Computer) kwa ajili ya kuboresha bidhaa zake..

Kifaa
Idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza kifaa cha kudarizi cha kisasa kabisa chenye vichwa nane kinacho tumia Computer, kitasaidia katika kukidhi mahitaji ya Ataba tukufu na vitengo vyake kwa kudarizi bendera, vitambaa na kila kitakacho hitaji kudariziwa, kawaida huhitajika vitu hivyo katika kipindi chote cha mwaka na hasa kipindi cha ziara na tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa maimamu watakasifu (a.s), pamoja na kuitikia maombi ya watu wanao kuja kufanya ziara wanao hitaji vitambaa vilivyo dariziwa hapa kwa ajili ya tabaruku.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa idara ya kudarizi Ustadh Munir Karaar Muhammad, kifaa hicho kitaongeza uzalishaji ulio kua unafanywa na mashine ndogo kuliko hiyo walizo kua nazo pia kitarahisisha utendaji na kuokoa muda, tutaweza kuzalisha bidhaa nyingi kwa muda mfupi na katika ubora mkubwa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeagiza kifaa hiki rasmi kutokana na maombi yetu kwao, miongoni mwa sifa za kifaa hiki ni:

“Kwanza: Kinafanya kazi kwa haraka kwa sababu kinavichwa nane, unaweza kuvitumia vyote kwa pamoja au kimoja kimoja.

Pili: Umakini wa utendaji kazi sawa sawa iwe ni kushona, kunakshi au kudarizi kwa sababu kimeonganishwa na tanakilishi (Computer) unaweza kuseti utakavyo.

Tatu: Kifaa cha kudarizi kina spidi (1200) kwa dakika.

Nne: Kimeunganishwa na program ya computer ambayo ni nyepesi kuitumia na rahisi kujifundisha, kina progrogram nyingi za ushonaji na kudarizi na unaweza kuongeza program nyingine yeyote na kuitumia.

Tano: Kipimo cha kipande kimoja katika kila kichwa ni (sm100) x (sm75).

Sita: Kinaweza kufanya na rangi tisa tofauti kwa wakati mmoja.

Saba: Unaweza kuitumia kwa kiasi chochote ukitakacho”.

Akaendelea kusema kua: “Kutokana na uzoefu wa idara ya ushonaji itaweza kukifanyia kazi kifaa hiki na kuifanya kudiriki aina zote za kiufundi, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu kazi inaendelea”.

Kumbuka kua idara ya ushonaji na kudarizi katika Atabatu Abbasiyya, inafanya kazi zote za kushona na kudarizi za Ataba tukufu, kuanzia kushona bendera iliyopo juu ya kubba tukufu na pazia zilizopo katika milango ya haram, pamoja na sare za watumishi na hushona kazi ya kitengo chochote miongoni mwa vitengo vya Ataba, hali kadhalika vitambaa na mabango na mengineyo, ilianza na mashine chache, kadri siku zinavyo ongezeka na haja inaongezeka pia na mashine zinaongezeka hadi kufikia sasa tuna idadi kubwa ya mashine na zinaendelea kuongezeka kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: