Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeenda kumtembelea muandishi wa habari raia wa Algeria Samira Muwaqi ambaye amelazwa katika mji wa Bagdad baada ya kujeruhiwa kichwani wakati akitekeleza majukumu yake ya kuripoti habari za kivita magharibi ya mji wa Tal-afar, ili kujiridhisha kuhusu maendeleo ya afya yake na kumsaidia katika mahitaji yake, kuonyesha namna wanavyo thamini kujitolea kwake na ushujaa wake katika kuripoti ukweli na ushindi unaopatikana kwa hashdi sha’abi na jeshi la serikali dhidi ya magaudi ya kidaesh.
Kingozi wa idara ya habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Khabaaz alisema kua: “Kutokana na maelekezo ya viongozi wakuu wa Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya; ujumbe wa ataba hizo umekuja kuangalia maendeleo ya afya ya muandishi wa habari raia wa Algeria Samira Muwaqi, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya mchango wake na ushujaa wake kwa kusimama pamoja na ndugu zake wapiganaji wa hashdi sha’abi na kuripoti ushindi wao na mihanga yao kivita na kibinadamu, na kurusha picha halisi ambayo haipatikani kwa waandishi wengi wa kuajiriwa, kutokana na msimamo wake magaidi walimtisha sana na wakamzuia asiingie katika maeneo yao, lakini aliendelea kubakia Iraq hadi amalize kazi aliyo anza ya kutangaza habari za kivita pamoja na hashdi sha’abi.
Akaendelea kusema kua: “Hakika mwanahabari Samira Muwaqi ni kielelezo cha haki na kujitolea, alisimama imara katika msitari wa mbele wa mapambano akavumilia matatizo makubwa na sauti kali (za mizinga) kwa sababu alitaka kuandika uhakika na kuufikisha kwa watu, tunatoa shukrani kubwa kwake na heshima ya hali ya juu tumekuja kutoka chini ya kubba mbili Husseiniyya na Abbasiyya (a.s) na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu mtukufu amponye haraka”.
Naye mwana habari Samira Muwaqi, aliisifu ziara hii na akashukuru sana ujumbe wa amani ulio mtembelea kutoka katika kubba takasifu katika aridhi tukufu, na akamuahidi Mwenyezi Mungu kua ataendelea kujitolea mpaka apate shahada kwa ajili ya nchi hii tukufu.
Kumbuka kua mwanahabari Mualgeria Samira Muwaqi alisifika kwa habari halisi kutoka ndani ya uwanja wa vita katika luninga (tv) zilizo sababisha mafanikio makuba, alikuja Iraq miezi michache kabla ya kuanza kwa vita ya kukomboa mji wa Mosul, alipigwa risasi ya kichwani na gaidi la kidaesh wakati akiripoti vita ya kukomboa uwanja wa ndege wa Tal-afar, ndipo akapelekwa hospitali, wakateuliwa madaktari bingwa kwa ajili yake, akiwemo bingwa wa macho na wa masikio, hakika alikua katika hali ya mbaya.