Baada ya udhibiti kamili wa miji inayo onganisha upande wa kulia wa Mosul na Tal-afar, kitengo cha uhandisi katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaanza kutegua mabomu ya aridhini yaliyo tegwa na magaidi wa daesh barabarani na katika majengo ya watu baada ya kuzidiwa katika midani ya vita, wamefanikiwa kutegua mabomu mengi na kuhakikisha usalama katika nyumba za watu, katika vijiji vya; Tal-kaisum, Sahaji na Khabirati, pia wamejenga ngome za kujilinda katika miji waliyo komboa toka kikosi cha 36 chini ya kikosi cha 9 kuanza vita vya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul.
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kusonga mbele katika vita hii, pamoja na kikosi cha tisa na vile vya jeshi la umoja na kikosi cha majibu ya haraka (radi sarii), wanaendelea na kusonga mbele kwa kufuata ratiba yao ya kijeshi, na wameweka maeneo matatu ya kijeshi ili iwe rahisi kuwasiliana baina yao, awamu hii ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul imeanza kabla ya saa 72 zilizo pita.