Baada ya kuongezeka kwa kazi katika vitengo vingine vya Ataba tukufu, uongozi wa Atabatu Abbasiyya ulitilia umuhimu sana katika kuboresha godauni ili iendane na vifaa inavyo tunza, makamo rais wa kitengo cha godauni Ustadhi Muhammad Niimatu Twaliqani aliuambia mtandao wa Alkafeel kua:
“Kitengo cha godauni -kama vilivyo vitengo vingine katika Ataba tukufu- visinge pata maendeleo waliyo nayo sasa kama sio kupitia katika zama ambazo tunaweza kusema zilikua za kujenga jiwe la msingi, ambapo kilianza kwa kufanya kazi ya kutunza vifaa, uongozi wa kisheria ulipo pewa madaraka rasmi kitengo hiki kilikua ndani ya ofisi yao, kwa kipindi kile kilikua kinatunza miswala, mikeka na baadhi ya vitu tofauti kama zawadi na misaada, kisha kazi zikaongezeka na umuhimu wake ukaongezeka, ilipo fikia kumiliki mali nyingi zinazo hamishika na zisizo hamishika ndipo idara kuu ikaona umuhimu wa kukifanya kua kitengo rasmi”.
Akaongeza kusema kua: “Kitengo hiki kina idara sita, kila idara inajukumu lake maalumu , idara zenyewe ni kama zifuatavyo:
- 1- Idara ya utawala:
Inahusika na mambo yote hasa kuandaa vitabu vinavyo toka na vinavyo ingia pamoja na mambo yote ya kiutawala, ikiwa ni pamoja na kusimaia godauni kwa kukagua kila kinacho ingia na kinacho toka na kupangilia gari za mizigo zinazo leta na zinazo toa, kazi hizi hufanya kwa ushirikiano wa sekta tatu; sekta ya watumishi, kamera na sekta ya usafirishaji.
- 2- Idara ya vitu vyote:
Inahusika na kutunza vitu vinavyo tumika mara kwa mara katika Ataba tukufu, na kupangilia uingiaji na utokaji wake, na inasekta zifuatazo: sekta ya vifaa vya majumbani (fenicha), sekta ya vifaa vya umeme, sekta ya mapambo na vioo, sekta ya vifaa vya ujenzi na sekta ya amanaati (kuwekeza kwa muda mfupi).
- 3- Idara ya miswala na vitu vya kutandika:
Inahusika na kutunza miswala ya Ataba tukufu na mavazi rasmi ya Ataba kama vile sale za watumishi na vinginevyo, pamoja na mablangeti, pia inafanya kazi chini ya sekta zifuatazo: sekta ya miswala ya viwandani, sekta ya miswala ya kutengeneza kwa mikono, sekta ya nguo, na sekta ya mablangeti.
- 4- Idara ya vitu tofauti:
Inahusika na kuhifadhi vitu vya dhamani na vifaa vya magari, na inasekta zifuatazo; sekta ya matumizi ya moja kwa moja, sekta ya mitambo (magari) na vifaa vya ufundi wa mitambo, sekta ya uchomeleaji, sekta ya vifaa vya hakiba, na sekta ya vitabu na machapisho.
- 5- Idara ya mauzo na vifaa vilivyo haribika:
Idara hii ilianzishwa kwa ajili ya kutatua tatizo la kukaa na kitu ambacho hakihitajiwi na Ataba tukufu, na inawezekana kukiuza, vitu vya aina hiyo huuzwa baada ya kufata taratibu za kisheria chini ya usimamizi wa kitengo cha mali za Ataba, idara hii ina sekta mbili; sekta ya mauzo na sekta ya mali zilizo haribika.
- 6- Idara ya usimamizi:
Inajukumu la kusimamia godauni zote na kutunza kumbu kumbu ya kila kinacho ingia na kutoka halafu wanajukumu la kuandaa ripoti inayo kabidhiwa mwisho wa mwaka inayo elezea maendeleo ya godauni na mali zote zilizopo ndani ya magodauni, idara hii inasekta zifuatazo: sekta ya mali, sekta ya ufatiliaji, sekta ya kuhesabu vutu vilivyo hifadhiwa, sekta ya hesabu kuu”.
Kuhusu eneo zilipo godauni na idadi ya watumishi Twalaqani alisema: “Tuna godauni nyingi, tuna godauni kajika jengo la Saqaau/2 katika kitongoji cha Ibrahimiyya, tuna godauni katika maegesho ya gari, na katika mtaa wa viwanda, kitengo hiki hadi sasa kina watumishi (123) katika idara na sekta zote tulizo taja, na wanaingia kazini kwa zamu mbili, zamu ya asubuhi na ya jioni”.
Baada ya kuangalia kazi na juhudi kubwa zinazo fanywa na ndugu zetu watumishi wa godauni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kiofisi na kiutendaji, tumeona uhalisia wa kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kwamba ni taasisi inayo kua, inafanya kila iwezalo kuhakikisha inaboresha kila sekta ili iweze kutoa huduma bora kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika kipindi chote cha mwaka.