Ugeni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu watembelea kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji waliopo katika eneo la Nakhibu..

Maoni katika picha
Ugeni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu ukihusisha masayyid na mashekhe watukufu jana siku ya Juma Nne ya (23 Jamadil Ula 1438h) sawa na (21/02/2017m) walitembelea kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji waliopo katika eneo la Nakhibu katika mkoa wa Ambari, kwa ajili ya kukagua hali zao na kuwapa msaada wa kimanawiyya na kimadiyya, hii ni miongoni mwa ratiba zake za kutembelea vikosi vya wapiganaji wa serikali na wale wa hashdi sha’abi tukufu.

Mkuu wa ugeni huo ambaye pia ni msaidizi wa rais wa kitengo cha dini katika Ataba tukufu Shekh Aadil aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na ratuba yake ya kutembelea wapiganaji watukufu wa vikosi vya aina zote, walipo katika msitari wa pele wa mapambano na wale waliopo katika maeneo yaliyo kombolewa kwa ajili ya kuwapa msaada wa kimanayya na kimadiyya, kama mnavyo fahamu; Marjaa dini mkuu anawapa wapiganaji umuhimu mkubwa sana, na tumefanya ziara hii kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ya kututaka tutembelea maeneo muhimu ya kijeshi, leo tumeamua kutembelea eneo la Nakhibu lililopo katika mkoa wa Ambar kwa sababu lipo mpakani na Karbala tukufu”.

Akabainisha kua: “Lengo la ziara hii ni kuwatembelea wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Swifiin wanao endesha shughuli zao kwa kushirikiana nao na kuwapa chakula pamoja na nguo. Tuliwakuta wakiwa na hamasa ya hali ya juu kabisa, hawana dalili yeyote ya uchovu bali kinyume chake, walikua wanasema: haitupi shida kubakia katika mapambano kwa saa, siku au miaka, jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunalinda amani ya watu wetu na kuhami arudhi ya nchi yetu kipenzi na maeneo yake matukufu kutokana na magaidi, na sisi tunasema inshallah bishara za ushindi kwa wairaq zimesha onekana, vita inayo endelea sasa huko Mosul ndio ya mwisho dhidi ya magaidi ya daesh na kwa sasa wanapumua pumzi za mwisho inshallah”.

Wapiganaji walishukuru sana kwa kuja kuwatembelea na wakasema hakika ziara hii inamaana kubwa sana kwao na inawajenga kimanawiyya zaidi.

Tunapenda kusema kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji katika uwanja wa vita na kutoa misaada kwao toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda hadi leo, kwa ajili ya kuhakikisha vita vinaendelea dhidi ya magaidi hadi ushindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: