Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaangusha ndege ya Daesh na chazuia shambulio la gari mbili zilizobeba vilipuzi..

Maoni katika picha
Kufatia vita inayo endelea ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wamefanikiwa kudondosha ndege katika kijiji cha Kaisum, iliyo kua imerushwa na madaesh ili kupiga picha vikosi vya kijeshi vilivyopo katika eneo hilo, lakini haikufanikiwa.

Kikosi cha anga cha jeshi la Iraq kwa kushirikiana na wapiganaji wa aridhini waliopo upande wa kulia wa Mosul wameshambulia moja ya ngome za magaidi wa kidaishi iliyo kua katika shule karibu na kijiji cha Sahaji waliyo kua wakitumia kushambulia maeneo yaliyo kombolewa, shambulio hilo lilipelekea kuuawa kwa magaidi (17) waliokua wamejificha humo.

Katika upande mwingine magaidi ya Daesh yalijaribu kufanya shambulio la kiuoga kwa kutaka kwenda kujilipua kwa kutumia magari mawili yenye vilipuzi mbele ya wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), wakawakuta majemedari wapo makini wakayazuia magari hayo mbali na wao na kuyalipua, tukio hilo limetokea katika kijiji cha Sahaji.

Nacho kikosi cha wahandisi kimefanikiwa kutegua mabomu katika gari moja lililo achwa na madaesh katika kijiji cha Talkaisum na lingine wakalilipua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: