Idara ya mahusiano na vyuo vikuu kwa kushirikiana na idara ya mahusiano ya harakati za Qur’an ambazo zipo chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu zimekamilisha semina ya kujenga uwezo wa walimu wa maarifa ya Qur’an katika vyuo vikuu vya Iraq, semina hii ni miongoni mwa semina za kitaalamu ambazo hufanywa na idara hii, hulenga kuongeza kiwango cha elimu kwa walimu wa Qur’an na kubadilishana mawazo katika mambo yanayo husu Qur’an tukufu, pia semina hii ililenga kufanyia kazi mapendekezo yaliyo tolewa katika kikao cha mwisho cha wakuu wa vyuo na wakuu wa vitengo vya maarifa ya Qur’an katika vyuo vikuu vya Iraq kilicho fanyika katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Hafla ya kuhitimisha ilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ilifanyika katika ukumbi uliopo kwenye jengo la imamu Mahadi (a.f) pia walihudhuria wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na washiriki wa semina ambao idadi yao ilifika (25) kutoka katika vyuo tofauti vya Iraq.
Simina hii ambayo tunatarajia kufatiwa na semina zingine, ilijikita katika kusomesha hukumu za usomaji wa Qur’an tukufu kinadharia na kivitendo, mkufunzi alikua ni dokta Raafii Aamiriy pia kulikua na mihadhara ya kidini kuhusu maendeleo ya binadamu, pia kulikua na vipindi vya majadiliano ambapo washiriki walijadiliana mambo mbalimbali kuhusu maarifa ya Qur’an tukufu na tafsiri yake, semina ilidumu siku nane, saa sita za darasani kila siku.