Barozi wa Brazil nchini Iraq: Miradi ya Atabatu Abbasiyya ni mizuri na inaleta fahari..

Maoni katika picha
Barozi mpya wa Brazil nchini Iraq (Mh: Siri Mighil Dimaghalhaiz) amesisitiza kua miradi ya Atabatu Abbariyya ni mizuri sana na inaleta fahari, ukizingatia kua inatekelezwa na mikono ya wairaq wenyewe.

Aliyasema hayo katika ziara aliyo fanya jana siku ya Juma Tano (24 Jamadil Ula 1438h) sawa na (22/02/2017m) na akakutana na viongozi tofauti na kutembelea baadhi ya miradi akiwa pamoja nao, miongoni mwa miradi aliyo tembelea ni: mradi wa upanuzi wa Ataba, mradi wa upauaji, mradi wa mawasiliano na kamera za ulinzi, na alimalizia kwa kutembelea makumbusho ya Alkafeel.

Mtandao wa Alkafeel ulikua pamoja nae katika matembezi hayo na ulipata nafasi ya kuongea naye, alikua na haya ya kusema: “Hii ni ziara yangu ya kwanza katika mji mtukufu wa Karbala toka nilipo chaguliwa kua balozi wa Brazili nchini hapa, nina furaha kubwa sana leo kutembelea mji wa Karbala tukufu, mji ambao unaheshima kubwa sana katika dini na huja kuutembelea mamilioni ya watu kila mwaka kutoka nchi mbalimbali, nimebahatika kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi wa upanuzi, upauaji, mitambo ya mawasiliano na kamera za ulinzi, miradi yote nimeikuta ipo katika ufanisi wa hali ya juu kabisa kwa kweli ni fahari kubwa ukizingatia kua miradi yote inaendeshwa na wairaq wenyewe, hii inanipa picha nzuri kuhusu mji huu na Ataba zake tukufu tofauti na habari zinazo tangazwa na baadhi ya vyombo vya habari”.

Akabainisha kua: “Katika ziara hii tumejadiliana mambo mbalimbali kuhusu uchumi na namna ya kushirikiana hapo baadae, kuhusu makumbusho ya Alkafeel ya vifaa kale na nakala kale, hakika tumeona vitu ambavyo ni nadra kuviona, historia yake inarejea katika zama tofauti, hali kadhalika tumeshuhudia mpangilio bora na namna nzuri ya uoneshaji wa vitu ambayo inashinda maktaba nyingi za duniani, natoa shukrani za dhati kwa watumishi wa Ataba tukufu na wasimamizi wa miradi kwa mapokezi mazuri waliyo nipatia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: