Kutokana na ugumu wanao pata baadhi ya wabunifu katika kutuma vielelezo vyao vya ubunifu kwa ajili ya kushiriki katika kongamano na maonyesho ya wabunifu wa kiiraq yatakayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeongeza muda wa kupokea vielelezo hivyo hadi tarehe (27/02/2017m) pia mnaweza kupeleka moja kwa moja katika ofisi zetu zilizopo Bagdad, au kutuma katika mtandao: https://alkaleel.net/ifi au barua pepe: (Scahc155@yahoo.com) na (Aiexcon2017@gmail.com) kwa maelezo zaidi piga simu: (07730907902 au 07813764052 au 07700478333).
Lengo la kongamano na maonyesho haya ni:
Moja: kusaidia na kushajihisha akili za wairaq katika kugundua ubunifu na kulea vipaji.
Pili: kuchangia katika kufanya tafiti na ubunifu na kuingiza katika uwanja halisi wa matumizi na kufikia malengo ya muda mfupi au mrefu.
Tatu: kunufaika na ubunifu wa watalamu wetu na kuuingiza katika soko la uchumi la hapa nchini.
Nne: kuchangia katika kuboresha uchumi wa Iraq kwa kutumia wabunifu na watalamu wetu.
Tano: kuchangia katika kuwaingiza watalamu na wabunifu katika hatua ya utendaji.
Sita: kunufaika na ubunifu wa kiviwanda na kuuingiza katika teknolojia ya uzalishaji.
Saba: kujenga uwelewa na utamaduni wa kuwajali wabunifu na kuijulisha jamii ya wairaq umuhimu wa kuwathamini wabunifu na ubunifu wao.