Idara ya mahusiano na vyuo yatafuta namna ya kusaidiana na kushirikiana na uongozi wa malezi wa Misan..

Maoni katika picha
Katika tukio ambalo sio la kwanza la kufungua milango ya mawasiliano na vituo vya kielimu na kimalezi katika mikoa ya Iraq, na kujadili njia na zana zinazo weza kuboresha elimu, na kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo yanayo weza kuboresha sekta ya malezi, ugeni kutoka katika idara ya mahusiano ya vyuo chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya ziara katika uongozi wa idara ya malezi ya mkoa wa Misan.

Ustadhi Azhari Ally Rikabi kiongozi wa idara ya mahusiano na vyuo alisema kua: “Ziara hii ni miongoni mwa harakati za idara, hufanya ziara kama hizi katika kipindi chote cha mwaka, pia hatuja wasahau wanafunzi wa shule za msini na za upili (sekondari) O levo na Alevo kwani wao ndio msingi ambao hujengwa juu yake aina zote za elimu, tunatarajia ziara hii iwe ni chachu ya kusaidiana na kushirikiana hapo baadae, miongoni mwa mambo yaliyo pendekezwa na kujadiliwa ni:

Moja: kuwasiliana kwa ajili ya kushirikiana na kuingiza wanafunzi wa mkoa huu katika mashindano ambayo huandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Pili: kuendesha semina chini ya usimamizi wa wakufunzi waliobobea katika mkoa wa Karbala au Misan.

Tatu: kufanya semina na kuweka hema za Scout kwa wanafunzi wa Misan.

Nne: kujadili mambo ya kitamaduni kwa wanafunzi.

Tano: kupokea ugeni wa wanafunzi na kimasomo katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa kituo cha malezi cha mkoa wa Misan Ustadhi Riyadh Mujbalu Saaidiy ameonyesha kuridhika na mapendekezo haya ambayo manufaa yake yanarejea katika ofisi ya malezi ya mkoa wa Misan.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: