Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu uliyo somwa na Muhammad Muhsin Jauan mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Qur’an tukufu, kisha ukafatia ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliosomwa kwa niaba na mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi, alianza kwa kutoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikisha kwa mashindano haya, na akasema: “Hakika walio hifadhi Qur’an tukufu wana hadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, imebainishwa na aya za Qur’an na kusisitiziwa na hadithi za maimamu wa Ahlulbait (a.s), mtu aliye hifadhi Qur’an anamalipo makubwa hulipwa pia mwalimu aliyemfundisha na kumsaidia aweze kuhifadhi Qur’an na wazazi wake walio mshajihisha, mashindano haya ni kwa ajili ya kujenga moyo wa kuongeza juhudi katika kuhifadhi, yamefanikiwa katika mpangilio wake na ushiriki pia siku za mbele mtashuhudia mashindano kama haya ya walio hifadhi Qur’an nzima”.
Akaongeza kua: “Hakuna aliye feli katika mashindano haya, wote mmefaulu mmepata malipo makubwa na mtaendelea kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa”.
Baada ya hapo yalifanyika maonyesho ya kuhifadhi Qur’an tukufu na wanafunzi walioshiriki katika mashindano, alianza Mustafa Saaduni ambaye amehifadhi juzuu ishirini, kwa kuulizwa maswali na wahudhuriaji, walimuuliza aya ya kwanza katika sura na yeye akawa anasoma aya zinazo fuata hadi mwisho, kisha akafuata Ali Raadi Muhammad aliye hifadhi juzuu tatu, pia aliulizwa na wahudhuriaji kwa kusomewa aya na yeye anataja namba ya aya hiyo, sura na ukurasa kisha anaisoma na anaendelea kusoma aya zinazo fuata.
Halafu kulikua na ujumbe wa majaji uliosomwa kwa niaba na jaji wa Qur’an Ustadh Qassim Hami, alisema kua: “Hakika mashindano haya ni sawa na mashindano ya kitaifa, kutokana na namna yalivyo endeshwa, hii ni kutokana na juhudi zilizo fanywa na Maahadi pamoja na kituo cha kuandaa wasomi, kimeweza kutuletea mahafidhi bora watakao wakilisha Iraq katika mashindano ya kimataifa, shukrani za dhati ziwaendee washiriki na walimu wao, kamati ya majaji imetumia utaratibu unao tumika hapa Iraq na nje ya Iraq, na Maahadi iliweka masharti mazuri sana yamewasaidia mahafidh kuendeleza vipawa vyao na kusoma kwa kufuata hukumu, hakika zoezi lilikua zuri na litakua na mustakbali mzuri”.
Kisha kamati ya majaji walitangaza majina ya walioshinda na kuwapa zawadi, washindi walikua kama wafuatavyo:
Walio hifadhi juzuu moja:
- 1- Amiri Ahmadi Aajil
- 2- Mustafa Muhammad Jafari
- 3- Ali Karari Swalehe
Walio hifadhi juzuu tatu:
- 1- Muhammad Hussaam Muhsin
- 2- Mussa Faiz Qassim
- 3- Ali Raadu Muhammad
Walio hifadhi juzuu tano:
- 1- Ibrahim Maitham Muhammad
- 2- Wasam Khawaam Abdulkadhim
- 3- Muqtada Mushtaqu
Walio hifadhi juzuu kumi:
- 1- Sajadi Hussein
- 2- Abbasi Haidari Muhammad
- 3- Murtadha Raid Awadi
Walio hifadhi juzuu kumi na tano:
- 1- Haidari Falihu Rashidi
- 2- Hussein Anisi Muhsin
- 3- Halikutajwa jina lake kwa kutopata max zilizo takiwa
Walio hifadhi juzuu ishirini:
- 1- Hassan Muhammad Jaasim
- 2- Muhammad Alawi Hassan
- 3- Mustafa Saaduni Jaabir