Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea na semina za (kumtambua mwalimu mwenye mafanikio) kwa walimu kutoka mikoa tofauti..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na semina za kujenga uwezo wa walimu kutoka katika mikoa mbali mbali ya Iraq, na semina ya mwisho ni ile iliyo fanywa na idara ya uhusiano na vyuo kwa walimu wa kike katika mkoa wa Basra, ilidumu siku tatu na walishiriki zaidi ya walimu ishirini.

Hafla ya kukamilisha semina ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu na kufuatiwa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Aadil Wakil kutoka katika kitengo cha dini, miongoni mwa aliyo sema ni: “Tunapo zungumzia malezi hua tunazungumzia kitu chenye uzito mkubwa katika jamii, wala sitafuni mateno katika hili: hakika binti zetu wanaiga kutoka kwenu zaidi ya wanavyo iga kutoka majumbanu mwao, kuna walimu wa kike wamewalea mabinti malezi mazuri kabisa pamoja na kua ni wanafunzi, lakini wamejitahidi na kufanya kila aina ya juhudi kuhakikisha anamlea binti vizuri, kwa kweli wamefaulu katika upande wa masomo ya kisekula na katika upande wa tabia nyema na dini, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu tunasema: Hakika binti zetu ni amana kwenu lazima itunzwe na kuhifadhiwa”.

Akaongoza kua: “Hakika mwanafunzi anapokea elimu kwa umakini mkubwa sana kutoka kwa mwalimu wake mlezi, hasa hapa Iraq watoto wetu wana uelewa mkubwa sana, uwelewa huo unahitaji malezi, kwa kweli tunawaambia kua: kwa utukufu wa juhudi zenu, tunataka kuona kizazi kizuri chenye maendeleo makubwa ya kijamii, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akupeni taufiq na msimamo inshallah mlitumia muda kukaa katika mji wa Karbala aridhi ya Hussein na Abbasi (a.s)”.

Kisha ukafuatia ujumbe wa walimu ulio wasilishwa na Ustadhat Asmaau Khuzaai ambaye alisema kua: “Sisi tupo katika ardhi tukufu, tunapamba macho yetu kwa kumuangalia mbora wa watoaji na wenye kujitolea, tumeacha miji yetu na familia zetu kutokana na shauku yetu kwa kaaba ya nyoyo na kibla ya wapenzi (wa Ahlulbaiti as), hakika tumepata chakula cha moyo, mawaidha bora, fikra mpya zenye kujenga utumikaji na moyo wa kujitolea, tulifungua milango kupakea chakula cha roho na kuongeza elimu hakika tumepata kilicho bora kabisa kinacho maliza kiu ya nafsi, mmetupa mlicho nacho tena kwa njia rahisi mno, hakika mme mwagilia bustani na imestawi, tunatanguliza shukrani kwa Mwenyezi Mungu mtoaji wa neema kwa kuturahisishia swala hili na kuwafanyia wepesi walimu walio jitolea kututumikia kwa ushujaa mkubwa, kwa niaba ya wageni natoa shukrani ya pekee kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa wataalamu wake walio endesha semina hii ya kutujengea uwezo, hakika vizazi ni amana iliyopo katika shingo zetu, tukumbuke daima ujumbe wa mwalimu unafanana na ujumbe wa mitume”.

Mwisho kabisa viligawiwa vyeti vya ushiriki kwa walimu wanasemina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: