Atabatu Abbasiyya tukufu yazindua mradi wa shamba la mfano katika kilimo cha tende..

Maoni katika picha
Iraq ni miongoni mwa nchi zilizo kua katika daraja la kwanza kwa uzalishaji wa tende bora, ilikua inazalisha zaidi ya aina mia moja za tende, ukifuatilia swala hili utakuta ilianza kushuka siku baada ya siku hadi imekua miongoni mwa nchi zilizo baki nyuma kabisa katika kilimo hicho, bali hata idadi ya tende imepungua sana, mashamba ya tende imekua ni sehemu za makazi au mashamba ya mazao mengine au viwandani (hakuna mashamba maalumu kwa ajili ya mitende), mkoa wa Karbala tukufu huchukuliwa kua miongoni mwa mikoa inayo lima tende, katika miaka ya karibuni umeshuka sana, yawezekana kwa sababu ya mashamba ya tende kubadilishwa na kua sehemu za makazi, kutokana na sababu hizo Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kulima shamba la mfano la mitende ya kisasa kwa ajili ya kuhifadhi zao hili, pia kunufaika na jangwa kubwa ambalo limekaa bure na kulibadilisha kua kijani kibichi, kama sehemu ya kufanyia kazi hadithi isemayo (Aridhi ni ya atakaye ihuisha).

Mradi huu umekuja kukamilisha mradi mwingine, ambao ni mradi wa kumwagilia kwa kutumia maji mbadala, sio maji ya mto Furat, vimechimbwa visima; tutatumia maji ya visima ambayo kwa mujibu wa tafiti yanafaa sana kumwagilia mimea ikiwemo mitende, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua mradi huu chini ya ushiriki wa kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ambaye alipanda mche wa kwanza kama ishara ya ufunguzi wa mradi huu.

Katika hatua ya kwanza mradi utatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa dunam (25) magharibi ya mkoa wa Karbala, kilometa (40) kutoka katikati ya mji, itapandwa aina nadra sana ya miche za mitende na inayo zaa nete nyingi, mradi huu unakusudia mambo yafuatayo:

Moja: Kunufaika na mashamba ya jangwani na kuendeleza kilimo katika mkoa wa Karbala.

Mbili: Mashamba haya ni kinga ya kimazingira kutokana na upepo na vimbunga vya udongo.

Tatu: Kuongeza fursa za ajira.

Nne: Kuchangia soko la kieneo kwa kuingiza tende mpya ambazo ni za nadra.

Tano: Kufanyia kazi uwezo wa watalamu wa kilimo.

Sita: Kunufaika na maji ya visima.

Saba: Uwezekano wa kulima miti mingine ya matunda.

Nane: Kuingiza vifaa vya kisasa katika kilimo cha tende na kunufaika na watalamu wa ndani na wa kimataifa.

Tisa: Kulifanya shamba hili kua msingi wa kupatikana kwa wingi aina za tende ambazo ni nadra (chache) sokoni.

Mradi huu ulitanguliwa na shughuli za utangulizi, miongoni mwa shughuli hizo ni:

  • 1- Kupata uhakika kuhusu uwezo wa udongo wa shamba, kwa kuchukua sampo za udongo kutoka sehemu tofauti na kwenda kuupima.
  • 2- Kuainisha eneo la ukubwa wa shamba la awamu ya kwanza ya mradi.
  • 3- Kusawazisha shamba na kuliseti.
  • 4- Kuandaa mashimo ya miche kwa kutumia kamba.
  • 5- Mradi kuupatia mtandao kamili.

Umiliki wa aridhi ya mradi huu ulikamilika kwa mujibu wa sheria za Iraq, katika ulimaji imetumika njia ya nne kwa nne, ambayo ni njia rahisi kiutendaji na katika uhudumiaji wa mitende hapo baadae, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuingiza vifaa maalumu vya utendaji, na mche unapandwa kila mwishoni mwa mraba wa nne, kuna kua na umbali kidogo kati ya mche na mche kama ilivyo pangwa awali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: