Kuongeza muda wa kupokea vocha za ushiriki wa mashindano ya Mahadawiyya ya tano.

Maoni katika picha
Kwa heshima ya siku za Mahadawiyya, katika kukumbuka kuzaliwa kwa imamu Hujja Almuntadhar (a.f) ndani ya mwezi mtukufu wa shabani, kamati ya maandalizi ya mashindano ya Mahadawiyya ya tano yanayo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kituo cha masomo ya takhasusi kuhusu imamu Mahadi (a.f) imeamua kuongeza muda wa kupokea vocha (copon) za ushiriki wa mashindano hayo.

Mwisho wa kupokea utakua siku ya Ijumaa (1 Shabani 1438h) sawa na (28/04/2017m) siku ya kupiga kura na kutangaza majina ya washindi itakua Ijumaa (22 Shabani 1438h) sawa na (19/ 05/2017m) wamesisitiza washiriki wajaze taratibu na wapate taarifa kamili kabla ya kuanza kujibu maswali ya mashindano.

Kumbuka kua mapato yatokanayo na mashindano haya yatapelekwa katika miradi ya Atabatu Abbasiyya na katika kusambaza tamaduni za Mahadawiyya, njia ya kushiriki mashindano haya nunua vocha (copon) ya ushiriki kwa kiasi cha elfu kumi dinari za kiiraq yenye maswali kuhusu imamu Mahadi (a.f) na utapata namba yoko, kisha itapigwa kura katika hafla ya kitaifa itakayo fanyika siku ya mwisho wa zoezi hili.

Zimeandaliwa zawadi (110) kumi za kwanza ni magari aina ya (Sotana) Saloon toleo la mwaka (2017) pamoja na namba ya gari, na zawadi mia ni safari za umra na kuzuru kaburi la mtume (s.a.w.w). vocha (copon) zinauzwa kwenye maeneo ya mazaru matukufu na katika vituo vya Ataba tukufu vya mauzo ya moja kwa moja, pamoja na katika vituo vya shirika la Nurul Kafeel vilivyo enea mikoani, kwa mujibu wa taarifa za kamati; mashindano yamepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu tofauti, wengi wameona kua ni njia nzuri ya kuelekeza watu katika mlengo sahihi, na inasaidia kujenga mahusiano mazuri kati ya Ataba tukufu na jamii ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: