Ziara yake katika hospitali ya Alkafeel, mshauri wa wizara ya afya hapa Iraq asifu maendeleo na kusema kua imekua miongoni mwa hospitali mashuhuri hapa nchini..

Maoni katika picha
“Hospitali ya rufaa Alkafeel ni miongoni mwa hospitali zilizo endelea, imekuo ni miongoni mwa hospitali mashuhuri hapa Iraq na katika eneo zima”.. haya yalisemwa na mshauri wa wizara ya afya ya Iraq dokta Abdul-amiri Mukhtaru katika ziara yake hivi karibuni, ambayo alipokelewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na naibu kiongozi mkuu wa hospitali dokta Swafaau Majidi Hamidi. Mshauri wa wizara ya afya alisikiliza maelezo kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali kupitia vitengo vyake mbalimbali, pamoja na maendeleo mapya yanayo fanywa na hospitali na miradi ya baadae ambayo inakusudiwa kuitekeleza.

Dokta Abdul-amiri Mukhtari alipongeza huduma zinazo tolewa na hospitali ya Alkafeel na akasema wizara ya afya ipo tayali kupokea maombi ya hospitali hii, akabainisha kua: “Hakika hospitali ya Alkafeel pamoja na kua ina umri mdogo lakini imekua mashuhuri hapa Iraq na katika ukanda wote, mafanikio inayopata yanatokana na juhudi kubwa na ufatiliaji unaofanywa na viongozi wa hospitali pamoja na viongozi wakuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu hasa katika upande wa vifaa tiba na upande wa kutafuta madaktari bingwa, hakika hospitali ya Alkafeel ina mchango mkubwa sana katika kusaidia hospitali za serikali, hususan katika kipindi hiki kigumu tunacho pitia kama nchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: