Kukamilika hatua ya mwisho ya mradi wa upanuzi wa haram katika upande wa upauaji wa ukumbi mtukufu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ametangaza kukamilika kwa hatua ya mwisho ya mradi wa upanuzi wa haram upande wa upauaji wa ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nayo ni kufunika paa la pili upande wa ndani kwa madini ya vioo (maraya) ya fasifsaiyya ambayo ndio hatua ya mwisho katika mradi huu.

Akaongeza kusema kua: “Fani ya vipande vya maraya ya fasifsaiyya ni miongoni mwa fani inayofanywa kwa miaka mingi na mafundi wa kiiraq, imekua ndio alama ya ujenzi wa mazaru za Iraq na miji mingine ya kiislamu, na Ataba za Iraq zimekua mashuhuri zaidi hasa za Karbala, kutokana na uzoefu wa miaka mingi kazi ya kuweka maraya wamepewa mafundi mahiri wa kiiraq”.

Akabainisha kua: “Kazi hii ilianza mwaka (2013m) ilihusisha uwekaji wa vipande vya paa la pili na kuweka mapambo ya upande wa ndani (katika dari la paa), kazi ilianzia upande wa mashariki ya Ataba tukufu sehemu ya mlango wa Alqami, kazi iligawanywa sehemu nyingi, kutokana na mpangilio ulio wekwa na shirika la kiiraq linalo tekeleza mradi, pia mradi huu ulihusisha kufunika mitambaa panya (daraja) ya chuma na sehemu za ndani ya kubba, baada ya kufunikwa awali kwa kuweka paa”.

Akafafanua kua: “Tulikua makini katika kuchagua aina za maraya na rangi zinazo endana na maeneo mengine ya haram tukufu, sehemu yote iliyo wekwa maraya inaukubwa wa mita za mraba (10,000) kazi hii imechukua muda mrefu kutokana na umaridadi katika uwekaji wa maraya hizo na wingi wa nakshi zake.

Akasema kua: “Uwekaji wa maraya hizi umefanywa kwa mikono na kwa kutumia gundi maalum, badala ya kutumia madini ya chokaa yaliyo kua yanatumika zamani katika fani hii, maraya zilizo tumika zina upana wa milimita 2 na ubora wa hali ya juu, rangi yake ni imara na zinavumilia mazingira magumu, ilichaguliwa gundi maalum ya aina ya (CNC) iliyo tengenezwa Holand kwa ajili ya kugundishia maraya hizi, kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la kiiraq linalo tekeleza mradi huu imethibitika kua zina uwezo mkubwa, na inachukuliwa kua ni miongoni mwa vitu muhimu vya kiufundi vilivyo ongezwa katika mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: