Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi ya azaa ndani ya ukumbi wake mtukufu kukumbuka shahada ya bibi Zaharaa (a.s)..

Maoni katika picha
Kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya mbora wa wanawake wa duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya majlisi za azaa katika ukumbi mtukufu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zilizo dumu kwa siku tatu, mihadhara ya kidini ilitolewa na Sayyid Muntadhar Haidari, alizungumzia dhulma alizo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s) na akafafanua namna alivyo pambana kwa ajili ya kunusuri ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Akabainisha kua: “Hakika bibi Fatuma (a.s) ana nafasi kubwa katika kujenga na kusimamia misingi ya dini ya kiislamu, bibi Zaharaa (a.s) ni tunu kutoka kwa Allah na zawadi ya Allah kwa mtume mtukufu (s.a.w.w), zaidi ya yote ni siri ya uimamu, na ndiye kuelelezo cha kuumbwa maimamu watakasifu (maasumina) (a.s), hadi leo uislamu umehifadhika kwa utukufu wake na uwepo wa imamu wa mwisho miongoni mwa maimamu wa uongofu Swahibu Zamaan imamu Mahadi (a.f), ambaye ni miongoni mwa baraka za bibi Fatuma Zaharaa (a.s), baada yake alipanda katika mimbari Mula Ammaar Samawi kwa ajili ya kusoma masaibu na matam.

Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi na yamewekwa mabango yanayo onyesha dhulma aliyo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s) katika ukumbi wa malalo matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na imepokea vikundi vya maombolezo vilivyo kuja kuhuisha tukio hili lenye kuumiza.

Tunapenda kusema hapa: kuna riwaya tatu tofauti zinazo elezea kufariki kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), alifariki mwaka wa kumi na moja hijiriya, kwa sababu mtume (s.a.w.w) alihiji hijja ya mwisho katika mwaka wa kumi na akafariki mwanzoni mwa mwaka wa kumi na moja, wanahistoria wamekubaliana kua bibi Fatuma Zaharaa (a.s) baada ya kufariki baba yake aliishi chini ya mwaka mmoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: