Kamati ya misaada katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea kutoa misaada kwa familia za wakimbizi..

Maoni katika picha
Kamati ya misaada katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeendelea kuzitembelea familia za wakimbizi ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kutoa misaada kwa wakimbizi kama sehemu ya kutekeleza agizo la Marjaa dini mkuu, hivi karibuni kamati ya misaada imezitembelea familia za wakimbizi wanaoishi katika husseiniyya zilizopo pembezoni mwa barabara ya Bagdadi – Karbala kwa ajili ya kuwapatia baadhi ya misaada ikiwemo vifaa vya umeme na mavazi pamoja na vitu vinginge.

Makamo rais wa kamati ya misaada Sayyid Abdurahmaan Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kamati ya misaada katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeendelea na utekelezaji wa ratiba yake ya kusaidia wakimbizi kama sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa dini mkuu ya kuzisaidia familia za wakimbizi, hivi karibuni kamati ya misaada ikiongozwa na kiongozi wake Sayyid Naafii Ni’ima Mussawiy imetembelea makumi ya familia za wakimbizi wanaoishi katika husseiniyya zilizopo pembezoni mwa barabara ya Karbala – Bagdad kwa ajili ya kuwapatia misaada ikiwa ni pamoja na vifaa vya umeme na nguo za wanawake na watoto pamoja na soksi za mikono”.

Akabainisha kua: “Kama mnavyo fahamu, Atabatu Abbasiyya tukufu haijaacha hata kidogo kutoa misaada kwa wakimbizi toka siku ya kwanza ya vita ya Mosul pamoja na miji mingine hadi leo, na tutaendelea kutoa misaada hadi tuhakikishe wakimbizi wote wamerejea katika nyumba zao”.

Familia za wakimbizi walitoa shukrani kubwa sana kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwatembelea na kuwapa misaada mara kwa mara.

Tunapenda kusema kua Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na wajibu wake wa ki-akhlaqi unaoendana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ya kusimama pamoja na wakimbizi kwa kuwapatia huduma za kibinadamu, imeundwa kamati maalumu ya kusimamia swala la watu wanaokimbia katika maeneo yenye vita, kwa kuwaandalia sehemu za kuishi na kuwapatia mahitaji ya lazima kadri ya uwezo wao katika kutekeleza hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: