Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kwa kushirikiana na kikosi cha tisa wamefanikiwa kukomboa kijiji cha Damiriji kusini mwa mji wa Badushi..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kusonga mbele katika vita ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul chini ya kauli mbiu (Tunakuja ewe Nainawa), majemedari imara jana siku ya Juma Tano (1 Jamadil Aakhar 1438h) sawa na (28/02/2017m) kwa kushirikiana na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamefanikiwa kukomboa kijiji cha Damiriji kilichopo kusini mwa mji wa Badushi na wakapandisha bendera za Iraq juu ya majengo ya serikali, baada ya mapambano makali yaliyo wapa hasara kubwa magaidi matakfiri ya daesh.

Siku za nyuma walitangaza kudhibiti milima ya Atwishana upande wa kulia na kushoto kwa ukamilifu, baada ya mapigano makali na kundi la kigaidi la daesh.

Kumbuka kua kushiriki kwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika vita hii ya kukomboa mji wa Mosul, kunatokana na uzoefu mkubwa waliopata katika vita mbalimbali walivyo shiriki pamoja na ndugu zao wa hashdi sha’abi na jeshi la umoja pamoja navikosi vingine vya kujilinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: