Machapisho tofauti: Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chashiriki maonyesho yanayo fanyika katika chuo kikuu cha Bagdad..

Maoni katika picha
Ketengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chashiriki maonyesho yanayo fanyika pembezoni mwa nadwa inayo endeshwa na kitivo cha Lugha katika chuo kikuu cha Bagdad chini ya anuani isemayo: (Mashambulizi wa mawahabi katika mji wa Karbala tukufu).

Ushiriki wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu ulihusisha machapisho mbalimbali yaliyo karibia aina (70) ikiwemo mausuaat (cd), vitabu na majarida yaliyo chapishwa na vituo vilivyo chini ya (Kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Basra, kituo cha turathi za Hilla na Maahadi ya Qur’an tukufu), maonyesho yalipata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki na wadau wa maonyesho.

Kituo cha turathi za Karbala tukufu kilikua na ushiriki wa aina yake katika nadwa iliyo endeshwa na chuo kikuu tajwa hapo juu, hali kadhalika kilipata muitikio mkubwa katika maonyesho hasa kutokana na picha (30) za mnato zilizo pamba korido yao, zilizo onyesha matukio mbali mbali ya mji wa Karbala tukufu, na mabango (14) yaliyo onyesha shambulio la mawahabi katika mji wa Karbala tukufu mwaka wa (1802h), ikiwa ni pamoja na baadhi ya picha za kuchora na ramani zilizo onyesha tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: