Ugeni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu watembelea wapiganaji waliopo katika msitari wa mbele dhidi ya adui..

Maoni katika picha
Ugeni kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio husisha massayyid na mashekhe wametembelea vikosi vya Hashdi Sha’abi vilivyopo katika msitari wa mbele dhidi ya adui, katika miji iliyo kombolewa hivi karibuni na wapiganaji wetu jasiri, ziara hii iliyo dumu siku nne imefanyika kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu aliye sisitiza kutembelea vikosi hivi kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi mkubwa walio pata hivi karibuni.

Kiongozi wa ugeni huo ambaye pia ni rais wa kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya Shekh Swalahu Karbalai aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita toka kutolewa kwa fatwa tukufu hadi leo na kuwapatia misaada mbalimbali, ziara hii imetokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.t), na tumetembelea vikosi mbalimbali vilivyopo mstari wa mbele katika miji iliyo kombolewa hivi karibuni kutoka mikononi mwa daesh na kuwapatia pesa kidogo pamoja na zawadi za kutabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Ziara hii imedumu siku nne na tumetembelea vikosi vya: (Liwaau Muntadhir, Saraya Aqida, Kikosi cha imamu Ali (a.s), kilicho chini ya Atabatu Alawiyya tukufu, Kikosi cha Sayyid Shuhadaau, Liwaau Khurasaani, Kikosi cha jeshi la Imamu, Liwaau Answaru Marji’ia, Liwaau Tufuf na jeshi la umoja) waliopo katika miji ya: (Ainu Jahash, Tal-faris, Samiir Ali, Tal-shanan, Tal-abatwa, Sahaji, Idaya na Hajafu) hali kadhalika tulitembelea vikosi vya Abbasi (a.s) na kikosi cha tisa cha cheshi la Iraq katika milima ya Atwishana na mji wa Sahaji, wapiganaji wote tuliwakuta wakiwa na hamasa kubwa sana”.

Akabainisha kua: “Vile vile tulitembelea hospitali ya Shaheed Swaaleh Bakhaati, ambayo ndio hospitali kubwa iliyopo karibu na maeneo ya vita, inatoa huduma za upasuaji na matibabu mengine kwa wapiganaji, tukawapa dawa zilizo kua ndani ya uwezo wetu, kisha tukatembelea kikao cha azaa ya shahid (Abuu Twaha Naaswiriy) mmoja wa viongozi wakubwa katika kikosi cha Badri, kilicho fanyika katika makao makuu ya kikosi hicho, tulipokelewa na Haji Hadi Al-amiliy pamoja na viongozi wengine akiwemo Hamid Almaaliki kiongozi wa kikosi cha anga pamoja na wana anga majemedali, wakiwepo na jopo la wanahabari za kivita katika mji wa Tal-faris, tukawapa baadhi ya zawadi za tabaruku, hakika naweza kusema kua wana anga wa jeshi la Iraq wanatoa ushirikiano mkubwa sana na vikosi vyote vya wapiganaji na wana mawasiliano ya hali ya juu kabisa”.

Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutembelea vikosi vya wapiganaji na kutoa misaada kwao, tangu ilipo tolewa fatwa tukufu hadi leo kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya magaidi waovu madaesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: