Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wahuisha shahada ya bibi Fatuma Zaharaa (s.a)..

Maoni katika picha
Hizi ni siku za machungu makubwa katika nyoyo za waumini, ni siku za kukumbuka kufariki kwa Swidiqa Twahira mbora wa wanawake wa duniani wa mwanzo na wa mwisho bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, inayo sema iliishi siku tisini na tano baada ya kufariki kwa baba yake Muhammad (s.a.w.w), kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu ikiwemo kufanya majlisi maalumu kwa watumishi wake.

Majlis ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu na kufatiwa na muhadhara uliotolewa na Shekh Muhammad Kuraitwi, ambaye alizungumzia dhulma alizo fanyiwa bibi Zaharaa (a.s), na akabainisha kua dhulma hizo huchukuliwa sawa na kufunguliwa kwa mlango wa masaaibu kwa Ahlulbait (a.s), akasema kua; hakika bibi Fatuma (a.s) ana hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa mujibu wa maneno ya mtume Muhammad (s.a.w.w) katika hadithi nyingi, miongoni mwa hadithi hizo ni: (Yeye ni roho yangu iliyopo kati ya pande zangu mbili) na (Fatuma ni pande litokanalo na mimi), pia mtume aliwataka watu waige tabia njema alizo pambika nazo bibi Fatuma (a.s), Shekh alizungumzia nutka muhimu kuhusu historia ya bibi Fatuma katika kueneza mafundisho ya uislamu.

Kumbuka kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila kona ya dunia wanakumbuka tukio hili la kufariki kishahidi kwa bibi Fatuma (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na mahala lilipo kaburi lake (a.s), hii inaonyesha wazi kudhulumiwa kwake na machungu aliyo pitia, hadi akaamua kumuhusia mumewe Amirul mu-minina Ali (a.s) afiche sehemu ya kaburi lake na jeneza lake lisishuhuduwe na yeyote miongoni mwa wale walio mdhulumu na kuchukua haki yake, alifariki akiwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya zenye nguvu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: