Mwaka wa pili mfululizo: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya mashindano ya kitaifa katika fani ya kuhutubu kwa wanafunzi wa shule za upili (sekondari)..

Maoni katika picha
Kufuatia ushindi wa wanajeshi yetu na hashdi sha’abi katika mkoa wa Mosul, hakika wameonyesha ushujaa mbubwa, asubuhi ya siku ya Alkhamisi (3 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (02/03/2017 m) katika ukumbi wa mikutano wa imamu Hassan (a.s) yamefanyika mashindano ya pili kuhusu fani ya kuhutubia na kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa wanafunzi wa shule za upili (sekondari), ikiwa ni miongoni mwa harakati za mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo kwa kushirikiana na viongozi wa vituo vya malezi katika mikoa ya nyanda za kati na kusini na kwa kuzishirikisha shule za maeneo hayo wameshiriki wanafunzi (45) katika mashindano haya.

Hafla ya mashindano haya ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur’an tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha maalum kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa mwimbo wa taifa na mwimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa (lahaja ya Ibaau), halafu ukafuatia ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Sayyid Adnan Jalukhan Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, alisema kua: “Leo hii tumekutana hapa sehemu takasifu kwa ajili ya kushuhudia mashindano ya utoaji wa hotuba (muhadhara) tukufu, ni muhimu kukumbuka sifa anazo takiwa awe nazo khatibu mwenye mafanikio, miongoni mwa sifa muhimu kabisa ni taqwa, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kuyafanyia kazi maneno anayo yasema, mzungumzaji anapo ongea jambo ambalo anataka kuliwasilisha kwa watu wengine anatakiwa jambo hilo alitekeleze yeye kwanza kabla ya kulifikisha kwa wengine, na jambo lingine anatakiwa kua na uwezo binafsi wa ufikishaji, mfano wa hilo; angalia uwezo binafsi wa ufikishaji aliokua nao bibi Zainabu (a.s) namna alivyo fikisha katika majlisi zilizo fanyika kwa Yazidi, pia khatibu anatakiwa aamini ujumbe anao ufikisha”.

Akaongeza kua: “Khatibu anatakiwa afahamu tamaduni zote na asome sana vitabu, ili ayapambe maongezi yake hadithi na riwaya tofauti pamoja na aya za Qur’an, pamoja na kuzingatia kiwango cha uwelewa wa watu wanao msikiliza, pia anatakiwa kuongea kwa lugha faswaha, hali kadhalika kuwe na uwiano wa maneno yake na kutikisika kwa mwili wake, pindi Khatibu anapo panda katika mimbari anatakiwa aongee kwa ulimi na kuchezesha mikono yake, kutikisa kwa mwili na mikono wakati wa kuongea ni lugha kubwa ambayo hupeleka ujumbe kwa msikilizaji”.

Baada ya hapo washiriki walianza kupanda katika mimbari mmoja mmoja, na kuwasilisha mada zao kama walivyo jiandaa, na wengi walizungumza kuhusu taifa hili kipenzi.

Kiongozi wa kitengo cha mahusiano na vyuo vikuu Ustadh Azhar Rikabi aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mada za mashindano haya zinahusu kuipenda nchi na kuwapongeza hashdi sha’abi, na mashindano yatachukua siku mbili, siku ya kwanza kutakua na vikao vya asubuhi na jioni na siku ya pili itakua ni hafla ya kuhitimisha kwa mashindano haya na kutangazwa majina ya washindi, washiriki wa mashindano haya wapo (45) kutoka katika mikoa tisa ambayo ni: (Karbala tukufu, Najafu Ashrafu, Bagdad, Qadisiyya, Baabil, Muthanna, Misaan, Waasit, Dhiqaar).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: