Miongoni mwa shamra shamra za kukumbuka kuzaliwa kwa mbora wa wanawake wa duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s), uongozi maalumu wa mazaru ya swahaba mtukufu Maitham bun Yahya Tammaar (r.a) wametangaza uzinduzi wa dirisha la aqida na utawalishaji la malalo matukufu siku ya Ijumaa (18 Jamaadil Aakhira 1438 h) sawa na (17/03/2017 m) katika uwanja mtukufu wa malalo hayo matakatifu.
Tammaar ni Abuu Salim Maitham bun Yahya mfanya kazi wa bani Muhammad Kufi Annahrawani, muuza tente katika mji wa Kufa, ndio akapewa jina la (Tammaar = Muuza tende), Maitham Tammaar alikua na elimu kubwa sana, na alikua miongoni mwa watu wa karibu na imamu Amirul mu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s) alikua msiri wake na hifadhio wa elimu yake, imamu Ali (a.s) alimfundisha mambo mengi na kumfungulia mambao yaliyo fichikana, miongoni mwa usia wa siri, kutokana na utukufu wake alikua anatajwa na mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katikati ya usiku mara nyingi, na alimuhusia wasii wake Murtadha (imamu Ali a.s) kuhusu yeye, na hii ni habari kubwa, inatuonyesha ukubwa wa hadhi ya Maitam (r.a).