Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu awatembelea wapiganaji wa kikoso cha Abbasi (a.s) na kupongeza ushindi wanao endelea kupata na kasifi ari zao..

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) amesifu moyo na ari waliyo nayo wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), na amepongeza ushindi walio pata katika vita vya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul chini ya kauli mbiu ya (Tunakuja ewe Nainawa). Aliyasema hayo katika ziara aliyo fanya akiongozana na jopo la wajumbe wa kamati ya uongozi pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendesha vita kali dhidi ya magaidi matakfiri ya daesh.

Ugeni huo ulipokelewa na kiongozi mkuu wa wapiganaji hao Ustadh Maitham Zaidiy na baadhi ya viongozi, ugeni uliwafikishia wapiganaji salamu na dua kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na watumishi wa Atabatu tukufu, na kupongeza ushindi wanao endelea kuupata.

Naye Ustadh Zaidiy alitoa maelezo kuhusu vita vinavyo endelea na mafanikio yaliyo patikana katika kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul dhidi ya magaidi ya daesh, ambapo hivi karibuni walikomboa milima ya Atwishana na maeneo ya pembezoni mwakwe, kikiwemo kijiji cha Darmiji kilichopo kusini mwa mji wa Badushi kwa kushirikiana na kikosi cha tisa cha jeshi la Iraq na sasa wanajiandaa na hatua zijazo.

Mwishoni mwa ziara; ugeni uliwahusia wapiganaji kuongeza juhudi na tahadhari, na kuhakikisha kua wanaendelea kuamilina vyema na watu wanaokimbia kutoka katika himaya ya daesh au katika maeeneo ya vita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: