Pamoja na kukaribia ufunguzi: Fahamu sifa za kiufundi za mradi wa upanuzi wa paa ya haram tukufu ya malalo ya Abulfadhl Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Hakika ujenzi huu umekua wa aina yake ukilinganisha na majengo mengine ya kiislamu, kila sehemu ilifanyiwa usanifu yakinifu na upembuzi makini na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, shirika linalo tekeleza mradi pamoja na viongozi wa waqfu Shia.

Miongoni mwa sifa za pekee zilizopo katika mradi huu ni:

  • 1- Paa bila nguzo:

Ujenzi wa aina hii umefanyika kwa mara ya kwanza, kuweka paa kubwa bila kutegemea nguzo za ndani ya ukumbi, baada ya muhandisi Hamid Swaaigh mkuu wa shirika linalo tekeleza mradi kuwasilisha michoro ya majengo ya paa na kupasishwa huu. Kutokana na kukosekana kwa shirika la kiiraqi lenye uzoefu na ujenzi wa aina hii tuliamua kufanya mazungumzo na mashirika ya (Hipro Technology) ya kimalesia yenye uzoefu mkubwa wa kujenga paa za aina hii, paa zenye kuwekwa miamba ya vyuma yenye urefu hadi wa mita 24 bila nguzo.

  • 2- Muonekano wa kubba na minara ya dhahabu na sehemu za juu ya haram:

Paa jipya la sasa linaruhusu kuona nje hadi asilimia %40, kwa kulifungua wakati unapo hitajika kwa kutumia mtambo maalum wa mtelezo (slide) unaotumia umeme, hili ni jambo jipya halikuwepo awali, program hii inajulikana kama kuangazia mchana kwa mwanga wa jua (Sky Light) vipande vya paa hufunguka na kuruhusu mtu aliyopo ndani kuona anga, hii ni kwa ajili ya kubakiza mazingira ya zamani japo kidogo pamoja na kuwekwa paa katika ukumbi huu.

  • 3- Uhalisia wa zamani na upya wa sasa.

Asilimia sitini (%60) ya paa jipya, upande wa nje limepambwa kwa kashi karbalai na upande wa ndani limepambwa kwa maqarnasat bagdadiyya (mapambo ya bagdadiyya) ya zamani na kufunikwa na maraya za Fasifasaiyya, uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu umezingatia kubakiza alama za ujenzi wa kiiraq na kiislamu wa zamani zilizo kuwepo, na kufanana kwa muonekano wa jengo la haram katika sehemu zake tofauti kunazidisha upekee wa jengo hili, pamoja na kuwepo kwa mbao nyepesi na imara zinazo endana na ubora wa paa hili, ikiwemo kuporeshwa huduma za utiaji baridi, mawasiliano, program za sauti (spika) zinazo saidia katika kuhudumia makundi ya maombolezo yanayo ingia katika ukumbi huu mtukufu, katika misimu ya Muharam, Safar na kumbukumbu za kuzaliwa na kufariki kwa maimamu watakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: