Idara ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha kwa mara ya tatu ratiba ya (marafiki wa maktaba) maadhimisho haya yanalenga kushajihisha usomaji, na huandaliwa na kusimamiwa na idara hiyo.
Yamefanyika katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s), na kufunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ikafuata hotuba ya kiongozi wa idara ya wanawake Ustadhat Ashwaaq Shadhir alisema kua: “Aliwahusia pande za maini yetu, mabinti wa mustakbali wamuige bibi Zaharaa (a.s) wamfanye kua kiigizo chema kwa kufuata mwenendo wake na kuiga tabia zake tukufu, na wasome uimara aliokua nao katika kuhami dini, hivyo waongeze juhudi ya kusoma elimu zote, dini, historian a hata elimu za sekula, hakika wao ni kina mama wa mustakbali na tegemeo la sasa”.
Baada ya hapo ilionyeshwa filamu inayo elezea muundo wa ofisi ya wakina mama na idara zake pamoja na harakati zao. Halafu kikafuatia kikao cha majadiliano kilicho shuhudia muhadhara kuhusu kuhama kwa mtume Muhammad (s.a.w.w) ulio tolewa na Ustadhat Lamyau Hussein Mussawiy, aliangazia baadhi ya vipengele katika tukio hilo la kihistoria ndani ya umma wa kiislamu, na mambo yaliyo fuatia baada ya kuhama kwa mtume katika historia ya kiislamu.
Kisha hafla ikamaliziwa kwa kutoa zawadi kwa washiriki wa ratiba ya marafiki wa maktaba.