Baada ya mafanikio makubwa yaliyo patikana kwa wapiganaji wa aridhini wa kikosi cha Abbasi (a.s) yaliyo pelekea kukombolewa maeneo makubwa yaliyo kua chini ya udhibiti wa magaidi ya daesh, kuna maendeleo mengine muhimu yamepatikana katika vikosi vya anga, ndege za kivita zisizo kua na rubani zimefanya shambulizi kubwa dhidi ya magaidi ya daesh.
Shambulizi hilo limetokana na taarifa za kina zilizo patikana kutokana na ndege za upelelezi za kikosi hiki cha Abbasi (a.s), baada ya kunasa harakati za adui magaidi ya daesh tuliwasambaratisha kwa kuwashabulia na kuwapa hasara kubwa ya watu na mali, na ndege zote zilirudi salama katika vituo vyake.