Baada ya miezi tangu isimame kufanya kazi: Hospitali ya rufaa Alkafeel yachukua jukumu la kutengeneza kifaa cha kupima maradhi ya moyo katika hospitali ya Hussein..

Maoni katika picha
Wataalamu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na jopo la wataalamu kutoka katika shirika la Falbas la Holand wameanza kutengeneza kifaa cha kupima maradhi ya moyo katika chuo cha hospitali ya Hussein (a.s), baada ya kupita miezi kadhaa bila kufanya kazi, huku wataalamu wa wizara ya afya wakiwa hawaja fanya juhudi yeyote ya kukitengeneza, jambo lililo sababisha kuathirika sana kwa wagonjwa wa moyo waliokua wakitegemea kifaa hicho.

Hospitali ya rufaa Alkafeel kwa kushirikiana na taasisi za serikali pamoja na wahisani wenye kuhisi majukumu na ubinadamu kwa wakazi wa Karbala, wameamua kubeba jukumu la kutengeneza kifaa hiki ambapo inakadiriwa kugharimu (30,683,000) dinari za kiiraq. mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel dokta Haidari Bahadeli alisema kua: “Kifaa hiki ni muhimu sana kuwepo katika kila hospitali, kuharibika na kusimama kufanya kazi kunasababisha usumbufu mkubwa sana kwa wagonjwa wa moyo, kutokana na umuhimu huo; tumeagiza wataalamu kutoka katika shirika la Falbas na kwa kusimamiwa na muhandisi wa idara ya ufundi ya hospitali na kuwataka wakitengeneze na kurudi upya kufanya kazi.

Akabainisha kua: “Hakika uchache wa bajeti ya serikali na uzito katika kuyaendea matatizo ya kibinadamu, yakiwemo ya kitabibu ndio sababu ya kuchelewa kutolewa msaada wa haraka na serikali katika kutengeneza kifaa hiki ambacho kina umuhimu mkubwa kwa wagonjwa wa maradhi ya moyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: