Kamati ya maandalizi ya kongamano la tano la Amirul mu-uminina (a.s) yatangaza kufanyika kwa kongamano na vipengele vyake muhimu..

Kauli mbiu ya kongamano
Kamati ya maandali ya kongamano la kitamaduni la Amirul mu-uminina (a.s), moja ya makongamano muhimu ambayo hufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu nje ya Iraq, katika nchi ya India, imetangaza kua awamu ya tano itafanyika katika husseiniyya ya utukufu wa wanawake (Fadhlu nnisaai) katika mji wa Kalkata tarehe (14 – 19) ya mwezi wa Rajabu (1438 h) chini ya kauli mbiu: (Amirul mu-uminina (a.s) ni hoja kwa waja na muongozaji katika wema) ikiwa ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mlango wa elimu ya mtume (s.a.w.w) imamu Ali (a.s), pamoja na kushiriki kwa Atabatu Abbasiyya pia watashiriki wajumbe kutoka katika Ataba zingine zikiwemo (Alawiyya, Husseiniyya, Kaadhimiyya na Askariyya).

Maandalizi ya kongamano hili yameanza muda mrefu kwa ajili ya kulinda mafanikio mazuri yaliyo patikana katika makongamano yaliyo pita, na yaliacha athari kubwa katika miji yaliko fanyika, (mara mbili yalifanyika katika mji wa Lankaar mfululizo na yakafanyika mara moja katika mji wa Haidari Abadi kisha yakafanyika tena katika mji wa Lankaar) jambo ambalo limepelekea miji mingine kuomba kua wenyeji wa kongamano hili.

Vipengele muhimu katika kongamano hili ni:

  1. Maonyesho ya vitabu kutoka katika Ataba za Iraq, huonyesha machapisho yao ya vitabu vya kielimu na kitamaduni.
  2. Kufanya vikao vya usomaji wa Qur’an tukufu kama ilivyo kua katika miaka ya nyuma, husomwa na wasomi wa kimataifa kutoka katika Ataba tukufu, hii ni sehemu muhimu kwa sababu wasomaji wakiiraq hasa wa Ataba wanamvuto mkubwa sana kwa waislamu wa India.
  3. Kutembelea husseiniya, misikiti, vituo vya mayatima na watu muhimu katika dini, na hili jambo ni muhimu katika kujenga mahusiano.
  4. Kufanya mashindano ya kiitikadi, hasa kwa matawi ya Ataba tukufu, kama inavyo fanyika kila mwaka.
  5. Kutolewa mihadhara ya kidini, kwa kuzungumzia baadhi ya historia ya imamu Ali (a.s) na kufanya visomo vya ziara na dua.

Matawi ya Ataba tukufu yatahusishwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa ratiba za kongamano, ikiwa pamoja na kuendesha harakati za ufunguzi na ufungaji, utoaji wa matamko mbali mbali na usomaji wa mashairi.

Kutakua na tukio lingine kwenye husseiniyya ya Karbala tukufu katika mji wa Sharnihi siku ya (19 Rajabu 1438 h), nalo ni tukio la kupandisha bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) kutakua na ratiba maalumu ya shughuli hiyo. Makatibu wakuu wa Ataba tukufu walipo pewa mialiko ya kushiriki katika tukio hilo walithibitisha ushiriki wao.

Kumbuka kongamano la kitamaduni la Amirul mu-uminina (a.s) hufanywa kwa ajili ya kuuenzi utukufu wa Ahlulbaiti (a.s) na kusambaza mienendo yao na historia zao tukufu ambazo zimeifundisha dunia maana ya uislamu wa kweli, na kuthibitisha nafasi kubwa iliyo nazo Ataba za Iraq katika kuendesha makongamano, nadwa na mikutano ndani na nje ya Iraq, kwa kufanya hivi wanakua wamefungua mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa jamii mbali mbali katika kushughulikia mambo yanayo husu madhehebu na kuelezea historia za Ataba tukufu, hatua za ujenzi wake, idara zake na namna zilivyo fikia katika kiwango cha kuonekana kua ni muongozo kwa watu wote na mfano mwema katika nyanja zote ndani ya jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: