Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji: Tumekomboa kilometa 300 katika siku 10 tumewapa somo daesh ambalo hawata lisahau na tupo tayari kwa awamu ya pili ya vita ya ukombozi..

Maoni katika picha
Kiongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji amesema kua: “Ndani ya siku kumi tumeweza kukomboa kilometa 300 kutoka mikononi mwa magaidi matakfiri ya daesh katika upande wa kulia wa mji wa Mosul chini ya kauli mbiu ya (Tunakuja ewe Nainawa), tumewapa somo kubwa na hasara ya hali ya juu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika majemedari wa Alkafeel na wanao shirikiana nao kikosi cha tisa cha jeshi la serikali, wamefanikiwa kuua magaidi (200) kwa kutumia siraha tofauti, vifaru, mabomu na siraha nyepesi, wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanaushujaa mkubwa na ujasiri wa hali ya juu, wanashindana katika kukomboa kila kipande cha aridhi hii tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Kwa mara ya kwanza zimeshiriki ndege za kivita zisizo kua na rubani za kikosi cha Abbasi (a.s) katika kuwaangamiza madaesh kwenye maeneo yao, na zimesaidia sana katika kukomboa miji ya Kaisum, Sahaji, milima ya Kawitwara na milima ya Atwishana vita vya maeneo hayo vilidhihisha ushujaa wa wapiganaji wetu”.

Vikosi vya wapiganaji wa Abbasi (a.s) na kikosi cha tisa cha jeshi la Iraq wanaendelea kusafisha miji waliyo ikomboa kwa kutegua mabomu ya aridhini na kuhakikisha usalama katika maeneo yote pamoja na upande wa magharibi wa jeshi la kupambana na magaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: