Kiongozi wa makumbusho Ustadh Swadiq Laazim aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Makumbusho inavifaa vizuri sana vya kifalme, vilivyo kua vikitumiwa na viongozi na watemi, miongoni mwa vifaa hivyo vipo vilivyo kua vinawekwa katika vilemba na vimetengenezwa kwa dhahabu pamoja na madini mbalimbali kama vile yakuti, zamrad na kioo cha kijani, wakatoa zawadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa wafalme waliotoa zawadi katika malalo haya ni; wafalme wa Kajaar, Swafawiyyah na Othmaniyyah na wengineo, ikiwa ni pamoja na aina mbalimbali za mapambo, mikufu na vifaa ambavyo ni nadra kuviona katika makumbusho mengine, vifaa hivyo vipo vya aina kuu tatu, ambazo ni: dhahabu, fedha, na mawe ya thamani, kama vile almasi, yaquut na zamrad”.
Akaongeza kusema kua: “Kuna vitu vingi vya thamani vilivyopo katika umbo la maua ya mimea vimetengenezwa kwa dhahabu na fedha na kupambwa kwa mawe ya thamani, vina majina tofauti, vingine huitwa (Burushati) na baadhi nyingine huitwa (Naadiriyya) kutokana na kunasibishwa kwake na mfalme Naadir Shaha wa Farisi, pamoja na mikufu ya dhahabu, mapambo ambayo huwekwa kichwani na vifaa vya wanawake vya dhahabu na fedha, hali kadhalika heleni za zamani kabisa, pia kuna vifaa vifuatavyo:
- 1- Kandili (taa) ya dhahabu halisi ina maandishi yaliyo nakshiwa yasemayo: “Wakfu wa imamu Abbasi a.s”.
- 2- Mikanda ya zamani iliyo tengenezwa kwa vitambaa vilivyo tiwa dhahabu na mina”.
Akaendelea kusema kua: “Makumbusho hii inapete nyingi na tasbihi za thamani, zilizo tengenezwa kwa mawe ya thamani kama vile Aqiqi na mengineo, pia kuna Aqiqi ya Japan na Yaquut na Zamrad, vilevile kuna vifaa vingi vilivyo toweka, lilibainika hilo baada ya kulinganisha vifaa vilivyo kuwepo mwaka wa (2000 m) na vilivyopo sasa hivi, tukakuta kuna vifaa vingi havionekani yawezekana vilipotea mwishoni mwa siku za utawala ulioambuka (wa Sadam)”.
Kuhusu namna ya utambuzi wa aina za mawe na utunzaji wake Ustadhi akafafanua kua: “Hutambua aina za mawe kwa kutumia wataalamu walio bobea katika fani hiyo, pia tuna kifaa cha kupima mawe na kutambua aina zake, na huyahifadhi mawe hayo kwa viwango maalumu vya kitaalamu”.