Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu chashirikiana na maktaba ya chuo kikuu cha Bagdad kuhuisha siku yake ya kila mwaka..

Maoni katika picha
Katika kuenzi uhusiano kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na vyuo vikuu vya Iraq na kwa ajili ya kufungua milango ya kushirikiana, kitengo cha habari na utamaduni kimeshiriki katika maonyesho ya mwaka ambayo hufanywa na maktaba kuu ya chuo cha Bagdad, kupitia tawi lake walio beba machapisho ya kielimu na kitamaduni yanayo faa tabaka la watu wa chuo walimu na wanafunzi.

Maonyesho yaliyo andaliwa na maktaba hiyo yatadumu siku kumi, vituo na taasisi za usambazaji wa vitabu zimeshiriki, pia imekua fursa nzuri ya kutangaza vitabu na machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na yanasifa ya pekee, kwani utunzi na uchapaji vyote vinafanyika ndani ya Ataba tukufu.

Rais wa chuo kikuu cha Bagdad dokta Alaau Abdulhuseein Abdurasul alipo tembelea tawi la Ataba tukufu alisema kua: “Juhudi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika machapisho yake na aina za machapisho hayo pamoja na maudhui (mada) zilizomo, zinachangia sana katika kuongeza kiwango cha utamaduni kwa wanafunzi sambamba na kiwango cha elimu wanayo ipata wanafunzi wa vyuo, vilevile hii ni nafasi nzuri ya kujenga ushirikiano wa kweli baina ya chuo na taasisi za kiserikali pamoja na za kiraia, hususan Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na uhusiano wake imara na vyuo kwa kufanya makongamano ya kitamaduni na kushiriki katika nyanja za maktaba ikiwa ni pamoja na harakati zingine za kielimu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki mara nyingi katika maonyesho na makongamano mbalimbali ndani na nje ya Iraq, inakaribia kuto kosekana ushiriki wake katika kongamano au maonyesho yeyote yanayo fanyika, kutokana na utaratibu iliyo jiwekea wa kusambaza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), na hupata muitikio mkubwa sana kutoka kwa wadau, na huongeza idadi ya vitu vinavyo onyeshwa katika kila maonyesho hua tofauti na maonyesho iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: