Ukarimu na huduma bora katika mgahawa (mudhifu) wa mwenye ukarimu Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ni mkongwe kuliko migahawa ya Ataba zingine, unanyoosha mkono wa ukarimu, na unafungua mikono yake kuwakaribisha wageni kama alivyo kua mwenyewe kielelezo cha ukarimu na kujitolea, unatoa chakula kama zawadi na shifaa kwa watu wanaokuja kumtembelea yeye na ndugu yake imamu Hussein (a.s) kama muendelezo wa kukamilisha ukarimu wake (a.s) alio uonyesha katika mapambano ya Twafu, alikua mnyweshelezaji wa watu wenye kiu katika aridhi ya Karbala.

Ili kufahamu zaidi kuhusu kazi za kitengo cha mgahawa (mudhifu) na huduma zinazo tolewa kwa wageni mtandao wa Alkafeel umeongea na rais wa kitengo hicho Ustadh Kadhim Abdul-hussein ambaye alisema kua: “Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi ni miongoni mwa migahawa kongwe katika ulimwengu wa kiislamu, historia yake inarejea katika miaka ya (1980 m), na baada ya kuanguka utawala uliopita (wa Sadam) ulifanyiwa matengenezo na kupangiliwa kiofisi, kwa rehema za Mwenyezi Mungu na baraka za mwenye ukarimu mgahawa (mudhifu) huu ukafunguliwa katika sura mpya, kama kitengo rasmi miongoni mwa vitengo vya Ataba tukufu, katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s) tarehe (3 Shabani 1424 h) na kuendelea kutoa chakula kwa watu wanaokuja kufanya ziara kama kawaida, juhudi za kupanuliwa kwa ukumbi wa mgahawa zikafanika, ulipo anza mradi wa upanuzi wa jengo la haramu tukufu, nao ukumbi wa mgahawa ukapanuliwa hadi kufikia uwezo wa kuingiza watu mia saba (700) kwa wakati mmoja, hapo awali ulikua unaweza kuingiza watu mia moja na hamsini tu (150), hivyo tunaweza kulisha watu karibia elfu kumi katika chakula cha mchana peke yake, na chini ya hapo kidogo katika chakula cha usiku”.

Akaongeza kusema kua: “Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wenye mapenzi makubwa katika nyoyo za watu wanaokuja kufanya ziara ukilinganisha na migahawa mingine ya Ataba za ndani na nje ya Iraq, unajitahidi kuhakikisha unatoa huduma bora zaidi kwa wageni wake, kupitia idara zake tano zinazo fanya kazi, ambazo ni:

  • 1- Idara ya utawala: Ina ofisi tatu, ambazo ni: (ofisi ya mali, ofisi ya vitabu na ofisi ya madereva), inajukumu la kupangilia mambo ya kiutawala na kusimamia manunuzi pamoja na kuhakiki vitu vinavyo wasilishwa, kusimamia maswala ya kipesa kwa kuwasiliana na kitengo cha mali pamoja na kupangilia zamu za wafanya kazi, na kufatilia maagizo ya kiutawala yanayo toka ofisi kuu ya Ataba tukufu, na mengineyo.
  • 2- Idara ya ukaribishaji: ina ofisi tatu, ambazo ni: (ofisi ya utawala na mapokezi, ofisi ya watumishi na ofisi ya kahawa ya kiarabu) idara hii inajukumu la kusimamia usafi katika maeneo yote ya mgahawa na kutoa huduma kwa wageni kuanzia wanapo ingia katika sehemu ya chakula hadi watakapo toka.
  • 3- Idara ya chakula: Ina ofisi tatu: (ofisi ya jiko, ofisi ya bucha na ofisi ya mikate) idara hii ina wapishi bingwa ambao hupika vyakula vizuri vya aina tofauti.
  • 4- Idara ya mauzo: huandaa chakula cha aina mbalimbali kwa watumishi wa Ataba na kuwauzia kwa bei ya punguzo kama itakavyo elekezwa na utawala mkuu wa Ataba tukufu.
  • 5- Idara ya hospitali ya Alkafeel: Ina jukumu la kuandaa chakula cha madaktari na wagonywa walio lazwa katika hospitali hiyo”.

Akabainisha kua: “Katika siku za kawaida tunalisha watu elfu tatu hadi elfu tano, huku siku za Ijumaa na siku za ziara maalumu hulisha watu zaidi ya elfu kumi katika chakula cha mchana tu, tulikubaliana kuanza kutoa chakula cha jioni pale ilipo tolewa fatwa ya jihadi ya kujilinda na Marjaa dini mkuu na tukaanza kuandaa wapiganaji, pia tukaanza kwenda kutembelea wapiganaji katika kila sehemu, na katika ziara za milionea hua tunalisha maelfu kwa maelfu ya watu, na hua tunakua na sehemu nyingi zaidi za kugawia chakula ikiwa ni pamoja na njiani kwa wale wanaokuja kwa miguu kutoka kila kona, hua tunaweka wagawaji wa vyakula katika kila njia inayo ingia Karbala tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Tumefungua migahawa kwa jina la Barakaat Alkafeel inayo uza aina mbalimbali za vyakula vizuri kwa bei rahisi, tulipo gundua kua watu wanaokuja kumzuru imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanapenda vyakula vya aina tofauti, mgahawa wa kwanza upo karibu na sehemu ya Hauraa (a.s) na mgahawa wa pili upo mwishoni mwa barabara ya Alqamiy”.

Kuhusu vyanzo vya mapato ya mgahawa (mudhifu) Ustadhi Kadhim alisema kua: “Vyanzo vya mapato ya mgahawa (mudhifu) vimegawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni pesa/mali tunazo pewa na idara ya Ataba tukufu, na sehemu ya pili ni zawadi na nadhiri zinazo tolewa na watu wanao kuja kufanya ziara. Kuna njia tatu za kuingia watu katika mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwanza: hugawiwa kadi (copon) za mgahawa kwa mazuwaru bila kuchagua kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nne katika ofisi zetu zilizopo karibu na mgahawa. Pili: kupitia kitengo cha zawadi na nadhiri, kila mtu anaye changia kitu chochote anapewa kadi yeye pamoja na familia yake ya kuingia katika mgahawa. Tatu: kupitia kitengo cha mahusiano, ambacho huingiza taasisi za mayatima, taasisi za kijamii, kitaifa na familia za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: