Baada ya vita kali: Majemedari ya kikosi cha Abbasi (a.s) na wapiganaji wanao shirikiana nao wamedhibiti jela ya Badushi na wamepandisha bendera za Iraq juu ya kuta zake..

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) na wa kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamefanikisha kudhibiti jela ya Badushi upande wa kulia wa mji wa Mosul katika oporeshen ya (Tunakuja ewe Nainawa), baada ya mapambano makali waliyo fanya vijana wa kikosi cha Abbasi (a.s) yaliyo onyesha ushujaa na ujasiri wao na kuwapa hasara kubwa ya roho na vifaa magaidi ya daesh.

Kwa mujibu wa habari zilizo ripotiwa kutoka kwa kiongozi wa oporeshen hii ya tunakuja ewe Nainawa Abdul-amiri Rashidi Yarallah: “Hakika kikosi cha tisa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) wamedhibiti jela ya Badushi na kupandisha bendera ya Iraq katika kuta zake pia wamefanya upekuzi katika nyumba za makazi za jela hiyo”.

Kwa upande mwingine; wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) pamoja na wa kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamewaua magaidi nane katika mapambano ya kukomboa kijiji cha Rihaniyya ambacho ni miongoni mwa vitongoji vya Badushi katika upande wa kulia wa mji wa Mosul, baada ya kuukomboa wamepandisha bendera ya Iraq juu ya majengo yake.

Hali kadhalika wapiganaji wa Abbasi (a.s) pamoja na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamefanikiwa kudhibiti barabara kuu inayo unganisha baina ya Badushi na Mosul na kuwazingira kiukamilifu magaidi ya daesh.

Upande wa huduma za kibinadamu, kikosi cha Abbasi (a.s) na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamepokea zaidi ya wakimbizi elfu moja kutoka katika mji wa Badushi na kupewa huduma na kituo cha Alkafeel cha kuhudumia wakimbizi. Wamepewa huduma za kimatibabu na chakula ndani ya kituo hicho kilicho weka kambi magharibi ya upande wa kulia wa mji wa Mosul.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: