Mwaka wa tisa mfululizo leo Alkhamisi (10 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (09/03/2017 m) jirani na malalo ya Amirulmu-uminina zimeanza harakati za maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo husimamiwa na Atabatu Alawiyya tukufu.
Maonyesho yamefunguliwa na katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Nizaar Hablul-matiin (d.t) akiwa pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu dokta Jamali Dabaagh na baadhi ya viongozi wa Atabatu Alawiyya tukufu, na ugeni wa heshima kutoka katika Atabatu Abbasiyya ukiongozwa na rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Hashim Mussawiy pamoja na wawakilishi wa Maraajii dini watukufu na wawakilishi na viongozi wa Ataba na Mazaru tukufu pamoja na kundi kubwa la wadau mbalimbali, wa dini, tamaduni, sekula na jamii waliokuja kushuhudia maonyesho haya.
Tukio hili lilitanguliwa na hafla ya ufunguzi iliyo fanyika ndani ya ukumbi wa haram tukufu na kufunguliwa kwa Qur’an kisha akaongea katibua mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu, Sayyid Nizaar Hablul-matiin: “Hakika maonyesho haya ya vitabu ya kimataifa katika mji mtukufu wa Najafu yamepambwa na vitabu tofauti vilivyo andikwa na wataalamu wa fani mbalimbali, ili kuyaleta pamoja mataifa na kubadilishana maarifa na kuwafanya wapenzi wa elimu wapate kitu bora, hakika maonyesho yanaongeza ukaribu baina ya viongozi, wawakilishi wa Ataba tukufu na mazaru na wawakilishi wa maraajii dini watukufu pamoja na wana jamii wote”.
Kisha akaongea rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Alawiyya tukufu Shekh Saadi Khaaqani, akassema kua: “Hakika elimu ina athari kubwa katika kufanya umma uonekane kua bora na kuufanya udumu, kwa kutumia elimu haki huhifadhika na uadilifu wa Mwenyezi Mungu hutendeka, hakika umma zilizo dumu ni zile zilizo andika na kutunza historia yao, amma wale ambao hawakuandika wameisha kwa kuisha zama zao na hawana athari yeyote iliyo baki, kutokana na imani ya watumishi wa Atabatu Alawiyya tukufu kua waandishi ndio wanao hifadhi elimu, Atabatu Alawiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni pamoja na wasaidizi wake wameandaa maonyesho ya tisa ya vitabu pembezoni mwa malalo matukufu ya Amirulmu-uminina (a.s) katika mji wa mafaqihi na maulamaa wa fani zote, mji ambao hautoi isipokua kizuri”.
Atabatu Abbasiyya kama kawaida yao katika maonyesho ya aina hii walikua na ushiriki wa aina yao, kimeshiriki kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu wakiwa na viabu vya aina mbalimbali, vya kidini, kisekula, kitamaduni na vinginevyo, pia kilishiriki kitengo maalumu cha watoto katika maonyesho haya.
Kiongozi wa maonyesho haya Ustadh Abdurazaaq Shaibaani alisema kua: “Katika maonyesho haya kuna zaidi ya majina ya vitabu elfu (50) vinavyo elezea mambo tofauti ya kidini na kisiasa pia kuna kitengo maalumu cha watoto, maonyesho yatadumu siku (10) vimeshiriki vituo vya usambazaji wa vitabu (230) vya ndani na nje ya nchi, vimeongezeka vituo (30) ambayo havikuwepo awamu iliyo pita, nchi zinazo shiriki ni: Kuwait, Iran, Sirya, Lebanon, Misri, Jodan, Canada na Uingereza”.