Kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza kuwasaidia watu wanaokimbia vita katika maeneo yao, ambao wanazidi kuongezeka siku hizi kutokana na vita inayo endelea, na kutokana na wajibu wa kibinadamu, kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wamefungua kituo cha Alkafeel kwa ajili ya kusaidia wakimbizi.
Kiongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidi alisema kua: “Kimefunguliwa kituo hiki karibu na mji wa Badushi upande wa kulia wa Mosul kwa ajili ya kusaidia wakimbizi ambao idadi yao inaongezeka kila siku kutokana na kuendelea kuzidiwa nguvu kwa magaidi matakfiri ya dashi yanayo wafanya raia kama ngao kwao, kama walivyo onyesha ushujaa wao katika uwanja wa vita na kuwashinda magaidi leo hii wanaonyesha ubinadamu wao kwa kuwahudumia ndugu zao wakimbizi, kituo hiki kilicho pewa jina la Alkafeel ndio sehemu ya kwanza ya kupokea wakimbizi kisha kuwasafirishwa katika mahema yaliyo andaliwa na serikali, toka kufunguliwa kwa kituo hiki tumesha pokea zaidi ya wakimbizi elfu moja”.
Akaendelea kusema kua: “Miongoni mwa majukumu yanayo fanywa na kituo hiki ni:
Moja: Kuwasaidia raia kutoka katika maeneo ya vita na kuwasindikiza hadi kwenye kituo.
Mbili: Kuwapa ushauri nasaha na kuwafanya wajihisi huru na kutambua kua wapiganaji wamekuja kuwakomboa dhidi ya makucha hatari ya daesh.
Tatu: Kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa au majeruhi.
Nne: Kupewa chakula mara tu wanapo fika kituoni, chakula hicho kinaandaliwa na mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Tano: Kuhakikisha kutojipenyeza magaidi ya daesh miongoni mwao.
Sita: Kuwapandisha katika vyombo vya usafiri na kuwapeleka katika maeneo yaliyo tengwa rasmi kwa ajili ya wakimbizi na kuwapa nafasi ya kukutana na kiongozi mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidi.