Ugeni wa heshima kubwa ukiongozwa na muwakilishi wa Marjaa dini mkuu ambaye ni kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.t) leo siku ya Alkhamisi (10 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (09/03/2017 m) umetembelea wapiganaji waliopo katika oporesheni ya (Tunakuja ewe Nainawa) inayo endelea upande wa kulia wa mji wa Mosul. Akiongozana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) na baadhi ya marais wa vitengo na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) aliupokea ugeni huo na akawapa maelezo kuhusu maendelea ya vita vinavyo endeshwa na kikosi hicho pamoja na washirika wao, akafafanua miji waliyo komboa kutoka mikononi mwa daesh na malengo ya mbele katika mapambano hayo.
Sayyid Ahmadi Swafi baada ya kuwafikishia salamu kutoka kwa Marjaa dini mkuu na kuwaombea dua wapiganaji pamoja na kuwapongeza kwa ushindi mkubwa walio pata, alisisitiza mambo yafuatayo: kulinda uhai wa raia na mali zao pamoja na mali za umma, na kushikamana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ambayo yana sisitiza vitu hivyo, na waendelee kusifika kwa tabia nzuru na ubinadamu ambayo ndio sifa kubwa anayo sifika nayo katika vita zote, pia alisisitiza kuendeleza ushindi na kua na tahadhari kubwa wanapo amiliana na daesh.
Pembezoni ya ziara hii kilifanyika kikao kati ya ugeni huu na waziri wa ulinzi wa Iraq Arfaan Hiyaali na kiongozi wa oporesheni hii ya (Tunakuja ewe Nainawa) Abdul-amiri Yarallah na baadhi ya viongozi na wakuu wa vitengo vya wizara ya ulinzi, pia alishiriki kiongozi mkuu wa Hashdi Sha’abi Haji Haadi Al-amiriy.
Tutakujuzeni zaidi tutakapo pata taarifa kutoka katika vyanzo rasmi…