Kituo cha kutafiti mambo ya Afrika katika Atabatu Abbasiyya tukufu chajadili matatizo na ufumbuzi wa misimamo mikali katika bara la Afrika..

Maoni katika picha
Kituo cha kutafiti mambo ya Afrika chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya warsha ya kwanza ya (Kujadili misimamo mikali na ugaidi katika bara la Afrika), asubuhi ya siku ya Ijumaa (11 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (10/03/2017 m) katika ukumbi wa Qassim bun Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo hudhuriwa na wasomi na watu wa sekula kutoka ndani na nje ya Iraq.

Warsha hii ambayo ni sehemu ya warsha nyingine itakayo jadili mambo kama haya, imefanyika kujadili mambo ya Afrika na kung’amua mambo yanayo shabihiana na mambo ya Iraq pamoja na kujadili swala la ugaidi ambalo inaonyesha asilimia kubwa ya viongozi wa magenge ya kigaidi wanatoka katika bara ya Afrika.

Warsha ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha akaongea Sayyid Hashim Awaadi mkuu wa kituo cha Afrika, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika zao la elimu kwa mtu anaye fanya utafiti kuhusu bara la Arfika utaona kuna udhaifu, sio udhaifu wa kielimu bali vitendea kazi na watu kutolitilia umuhimu swala hilo, huenda ni kwa sababu ya picha waliyo nayo waarabu kwa ujumla na wairaq kuhusu bara la Afrika”.

Akafafanua kua: “Kituo cha kutafiti mambo ya Afrika kimekua wazi kwa vyuo vikuu vya Iraq na vituo vya utafiti kwa ajili ya kustawisha utafiti wa Afrika na kuweka plani itakayo tuwezesha kuendesha mradi huu katika namna bora zaidi”.

Baada yake yakaanza majadiliano yaliyo ongozwa na Ust. Dkt. Khairi Abdurazaaq Khafaaji kisha (wachokoza mada) maustadhi na wasomi wa kisekula wakawasilisha maoni yao ya kitafiti, ilikua kama ifuatavyo:

Kwanza: Ust. Dkt. Qassim Muhammad Abedi, aliwasilisha utafiti wake kuhusu hali ya kisiasa kwa taasisi za kigaidi katika bara la Afrika, aliuliza maswali na akatoa njia ya utatuzi wa tatizo la misimamo mikali katika bara la Afrika na udhaifu wa nchi yanako anzishwa makundi ya kigaidi.

Pili: Ust. Dkt. Sahadi Ismaeel Khalili, utafiti wake ulihusu kufadhiliwa kwa magenge ya kigaidi katika plani za Marekani katika bara la Afrika kutokana na jografia ya bara hilo na kufungamana kwake na mashariki ya kati.

Tatu: Dokta Ali Farisi Hamidi utafiti wake ulihusu kufadhili makundi ya kijamii katika plani ya kuimarisha jamii za waafrika.. Saudia na Iran kama mfano.

Kisha ukafunguliwa mlango wa maswali, majadiliano na maoni mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, (wachokoza mada) watafiti wakawa wanajibu na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.

Kisha vikagawiwa Vidani na vyeti vya ushiriki, na warsha ikahitimishwa kwa maneno ya Dokta Ahmadi Muhammad Twanshi, mkuu wa kitivo cha Athari katika chuo kikuu cha Qadisiyya ambaye alisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa ufumbuzi wa matatizo yaliyo tajwa na warsha na kufanyiwa kazi swala hilo kwa kulipeleka kwa wahusika na wenye maamuzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: