Makongamano na harakati za kitamaduni zinazo fanywa na Ataba tukufu, za ndani au nje likiwemo kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s), yanachangia kutambulisha huduma zinazo tolewa na malalo haya matukufu kwa watu wanaokuja kufanya ziara (mazuwaru) na maendeleo makubwa yaliyopo hivi sasa katika sekta ya elimu na utamaduni.
Haya yalisemwa na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Jafari Mussawiy (d.t) wakati alipokua akipokea mualiko rasmi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu wa kumtaka kuhudhuria kongamano litakalo fanyika katika Husseiniyya ya Utukufu wa wanawake (Fadhilu Nisaai) katika mji wa Kalkata nchini India kuanzia tarehe 14 – 19 Rajabu 1438 h. chini ya kauli mbiu ya (Amirul Mu-minina (a.s) ni hoja kwa waja na muongoaji katika wema), katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mlango wa elimu ya mtume (s.a.w.w) imamu Ali (a.s).
Akaongeza kusema kua: “Hakika Ataba tukufu zimekua ni vituo vinavyo angaza nuru ya tamaduni bora na dini sahihi na kufikisha fikra za Ahlulbait (a.s) kwa walimwengu bila kutumia njia zinazo umiza na chuki (ta’asubu), jambo hili linahitajia baadhi ya vitu, makongamano, mikutano na matamasha ya kitamaduni ni miongoni mwa vitu vizuri vinavyo saidia kufanikisha jambo hilo, na matunda yake yamesho onekana. Kuendelea kwa kongamano hili ni ushahidi wa wazi wa njia nzuri inayo fatwa na Ataba tukufu chini ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Mwishoni mwa maneno yake alisema: “Tunaishukuru Atabatu Abbasiyya na viongozi wake, hakika wamekua mstari wa mbele daima katika kufanya mikutano na makongamano, tunaomba muendelee hivi na Mwenyezi Mungu awawezeshe kufikia malengo yenu katika miaka ijayo inshallah.
Kumbuka kua kamati ya maandalizi ya kongamano hili ilikua imetangaza kua maandalizi ya kongamano hili yalianza muda mrefu, kwa ajili ya kulinda mafanikio mazuri yaliyo patikana katika makongamano yaliyo pita, yaliyo acha athari kubwa katika miji yaliko fanyika (yalifanyika mara mbili katika mji wa Naklau na mara moja katika mji wa Haidar-Abaad kisha yakafanyika tena katika mji wa Naklau) jambo lililo pelekea miji mingine kuleta maombi ya kutaka miaka ya mbele kongamano hili lifanyike katika miji yao kwa idhini ya Mwenyeni Mungu mtukufu.