Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaongeza udhibiti katika nji wa Badushi na chateka zaidi ya magaidi ya daesh mia moja na kusaidia wakimbizi elfu ishirini..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali wameongeza udhibiti wao katika mji wa Badushi, kikosi cha Abbasi (a.s) kilifanya mashambulizi makali dhidi ya magaidi matakfiri madaesh na kuwapa somo ambalo hawata lisahau, baada ya kukata mawasiliano yao kabisa, kiliwamiminia mvua ya moto na kuwapa hasara kubwa sana ya roho na mali, kiliua idadi kubwa ya magaidi na kikafanikiwa kuteka zaidi ya magaidi mia moja (100) ambao kimewakabidhi kwa viongozi wa juu.

Pia wapiganaji wa Abbasi (a.s) walifanikiwa kuwakamata madaesh waliojipenyeza katika familia za wakimbizi, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa oporesheni ya (Tunakuja ewe Nainawa) zinasema kua; wapiganaji wanaendelea na safisha safisha ya kutegua mabomu katika vijiji na miji waliyo komboa, na sasa hivi wanaelekea kiwanda cha saruji (cement) cha Badushi, na wamefanikiwa kukomboa vijiji vyote vinavyo zunguka kiwanda pamoja na milima ya pembezoni mwake, na kuingia ndani ya mji wa Badushi na kukomboa baadhi ya maeneo na wanasonga mbele kuelekea Talla-risi, vilevile wamefanikisha kukomboa kijiji cha Jamasa na kijiji cha Hamidati na wamedhibiti upande wa magharibi wa mto Dujla na wanaendelea kusonga mbele, katika opoersheni hii wameua idadi kubwa ya magaidi na wameangamiza magari manne (4) yaliyo jaa vilipuzi na hazina tatu za mabomu na magari mawili yaliyokua yamebeba magaidi pamoja na kuangamiza hazina mbili za siraha za (BKS).

Vilevile katika upande wa kibinadamu wamefanya kazi kubwa sana, waliimarisha usalama katika njia za wakimbizi, kikosi cha Abbasi (a.s) kwa kushirikiana na kikosi cha tisa cha jeshi la serikali walitoa msaada kwa watu zaidi ya elfu ishirini ndani ya siku tatu za nyuma, ambao walipokelewa katika kituo cha Alkafeel cha kusaidia wakimbizi kilicho funguliwa hivi karibuni upande wa kulia wa mji wa Mosul, ambacho kinamaandalizi ya tiba, vyakula na magari ya kusafirisha watu na kuwapeleka katika maeneo salama zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: