Nuru za matukufu katika uhai wa Fatuma bint Hizam Alkilabiyya, ajulikanaye kama Ummul Banina (a.s)..

Maoni katika picha
Nyumba ya mtume ililea watu watukufu sana, miongoni mwa watu walio lelewa na kuishi katika nyuma hii tukufu ni mama mtukufu Fatuma bint Hizam, anaye julikana kwa jina la Ummul Banina, ambaye ndio mama wa Abbasi na ndugu zake (a.s), tupo katika siku za kukumbuka kufariki kwake. Ummul Banina ni Fatuma Alkilabiyya anatokana na Aali Waheed, familia yake ni katika watukufu wa waarabu na viongozi wao na walikua ni mashujaa maarufu, baba yake anaitwa Abul-mahli, jina lake kamilini: Hizam bun Khalidi bun Rabi’a.

Alilelewa (a.s) na wazazi wake wawili watukufu, waliojulikana kwa tabia njema na akili pevu, na Mwenyezi Mungu mtukufu alimtunuku upole, utaratibu, utakasifu, na roho nzuri, akamtuniku uelewa na akili ya hali ya juu, alipo kua (balekhe) akawa mfano bora kwa wanawake wote katika tabia nzuri, ndipo Aqil Bun Abuutwalib akamchagua aolewe na ndugu yake Amirul Mu-uminina imamu Ali bun Abuutwalib (a.s).

Wakati alipo taka imamu Ali (a.s) kuowa mwanamke anaye tokana na ukoo wa mashujaa na wakarimu, ili amzalie watoto wenye ushujaa wa hali ya juu, imamu Ali (a.s) alimuambia ndugu yake Aqil –alikua mtambuzi wa nasaba za waarabu- amtafutie msichana kutoka katika ukoo wa mashujaa, Aqil akamuambia ndugu yake: (Ndugu yangu wamuonaje Fatuma bint Hizam Alkilabiyya, hakika hakuna katika waarabu watu mashujaa zaidi ya baba zake), ndipo Aqil akaenda katika nyumba ya Hizam na akamuambia kua, nimekuja kumposa binti yako mtukufu aolewe na bwana wa mawasii Ali (a.s). Mzee Hizam akakubali na ndoa ikafanyika kwa kufata mahari ya sunna ya mtume (s.a.w.w) alipo muozesha mwanawe bibi Fatuma (a.s) ambayo ni dirham mia tano.

Ummul Banina (a.s) ni miongoni mwa wanawake watukufu walio zitambua haki za Ahlulbait (a.s), alikua mfaswaha, mnyeyekevu, mcha Mungu, mwingi wa kuabudu, kutokana na utukufu wake bibi Zainabu mkubwa (a.s) alikua anamzuru baada ya kurudi kutoka katika tukio la Twafu kama vile alivyo kua akimzuru katika siku za suku kuu, alijulikana mama huyu mtukufu kwa ubora wa tabia zake, na miongoni mwa sifa zake maarufu zaidi ni “Utekelezaji” aliishi na Amirul Mu-uminina (a.s) kwa ikhlasi kubwa, na akaishi baada ya kuuawa kwake (a.s) muda mrefu na hakuolewa na mwanaume mwingine.

Baada ya utumishi wake kwa bwana wa mawasii (a.s) na watoto wake maimamu wawili Hassan na Hussein (a.s), wajukuu wa mtume (s.a.w.w) ambao ni mabwana wa vijana wa peponi, na huduma yake kwa Aqila bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), baada ya umri mrefu uliojaa ibada na huzuni za muda mrefu, za kuuawa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, kuanzia kuuawa kishahidi kwa Imamu Ali (a.s) katika mihrabu yake, na kuuawa watoto wake wanne kwa wakati mmoja wakimlinda na kumuhami kibenzi cha mtume na bwana wa mashahidi imamu Hussein (a.s). baada ya mambo yote hayo ukafika wakati wa kifo chake tarehe kumi na tatu Jamadil Aakhira (64 h) akaelekea kwa Mola wake mtukufu na akazikwa (a.s) katika makaburi ya Baqii, karibu na Ibrahim, Zainabu, Ummu Kulthum, Abdullahi, Qassim na wengineo miongoni mwa maswahaba na mashahidi, kaburi lake lilibomolewa na manawaasib (matakfiri) pamoja na makaburi ya maimamu wa nyumba ya mtume mtukufu, imamu Hassan Almujtaba, imamu Ali bun Hussein Zainul-Abidina, imamu Muhammad bun Ali Albaaqir, na imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s).

Mwana mama huyu amekua na hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu na mtume wake pamoja na Ahlulbait (a.s), mtu yeyeto atakaye muelekea Mwenyezi Mungu mtukufu akamuomba haja zake kwa kupitia utukufu wa mama huyu hufanikiwa maadamu haja hizo sio za haramu na hazivuki mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Amani iwe kwako ewe mama mwema mtakasifu, mtekelezaji mwenye ikhlasi, uliye fata nyayo za mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika kutii sheria na mwenendo wa maisha, siku uliyo zaliwa na siku uliyo fariki na siku utakayo fufuliwa mbele ya muumba wako, pongezi kubwa kwa kila atakaye iga mwenendo wako miongoni mwa wanawake wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: