Makundi ya waombolezaji yaingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kutoa taazia kwa kufariki mama yake Ummul Banina (a.s)..

Maoni katika picha
Ummul Banina (a.s) alikua na hadhi kubwa sana, alikua shujaa, mkarimu na mwenye kujiamini, aliwapenda na kuwatii Ahlulbait (a.s), alimpenda sana na kumtii mume wake imamu Ali (a.s) alimnyenyekea na kumtumikia.. bali alikua ni mtushi wa Ahlulbait (a.s).

Kutokana na umuhimu wa kuzihuisha na kuzitukuza alama za Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kuhuisha minasaba ya Ahlulbait (a.s) na kila anaye fungamana nao, vimekuja vikundi (mawaakibu) vya maombolezo kutoka nje na ndani ya Karbala tukufu kwa mbeba bendera wa imamu Hussein (a.s), mtoto kipenzi wa Ummul Banina (a.s) Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kumpa pole ya kumbukumbu ya kufiwa na mama yake, wakiwa wamebeba bendera za huzuni na wakiimba qaswida za maombolezo zinazo elezea utukufu wa Ummul Banina (a.s), ukarimu wake na hadhi kubwa aliyo pewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, (hakika alikua mwanamke mtukufu aliye fahamu haki za Ahlulbait (a.s) pia alikua mfaswaha, mcha Mungu na mwenye kuipa nyongo dunia).

Amani iwe kwake siku aliyo zaliwa na siku alizo ishi na kuwahudumia kutokana na utukufu wake Ahlulbait (a.s) na siku aliyo enda kwa Mola wake akiwa ni mwenye subura, mwenye kupigana jihadi, aliwatoa watoto wake vipenzi, Abbasi (a.s) na ndugu zake, aliwaandaa akawasisitiza kubeba jukumu kubwa la kufatana na kumuhami bwana wa Bani Hashim imamu Husseis (a.s) katika safari yake tukufu ya kuihuisha dini ya babu yake (s.a.w.w).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo chake (a.s) ratiba hiyo imehusisha vitu vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: