Pamoja na vita kali inayo endelea ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul inayo sababisha kuongezeka idadi ya watu wanao kimbia mateso ya daesh, ambao idadi yao inazidi watu elfu moja, Atabatu Abbasiyya imetuma magari kwenda kuzisaidia familia za wakimbizi.
Kituo cha kusaidia wakimbizi cha Alkafeel kilicho funguliwa hivi karibuni na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) karibu na mji wa Badushi kimefanikiwa kusaidia zaidi ya wakimbizi elfu (11) kwa kuwapa huduma za awali, chakula, matibabu na zinginezo, sasa yanatumwa magari kwa ajili ya kwenda kusaidia kuwasafirisha hadi katika maeneo salama zaidi, yaliyo andaliwa rasmi na serikali kwa ajili ya kuhifadhi wakimbizi.