Ofisi ya idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kumbukumbu ya kufariki kwa Ummul Banina (a.s)..

Maoni katika picha
Ofisi ya wanawake kupitia jarida la (Riyadhu Zaharaa –a.s-) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kumbukumbu ya kufariki kwa Ummul Banina (a.s) kwa kuendesha nadwa siku ya Juma Pili (13 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (12 Machi 2017 m) chini ya kauli mbiu isemayo (Kwa imani yake alifikia daraja la juu kabika la ukamilifu) katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha kiongozi wa idara ya wanawake ustadhat Ashwaaq Shadhir akaongea maneno ya ukaribishaji, halafu ikaonyeshwa filamu iliyo elezea mambo muhimu yaliyo andikwa na jarida la (Riyadhu Zaharaa –a.s-) kuhusu mama huyu (Ummul Banina) mtukufu, tandu lianze kutoka hadi leo, ikafuatia qaswida ya kishairi kutoka kwa mshairi wa kibaharaini (Zaharaa Mutaghawi) iliyosomwa kwaniaba yake na Israau Haashim Mussawiy), kisha ukafanyika mjadala kuhusu historia na uhai wa mama mtukufu Ummul Banina (a.s), na kuangazia kujitolea kwake kuliko dumu katika historia, na baadhi ya michango ikatolewa na wakina mama ambao ni watumishi wa idara hii.

Hafla ilikhitimishwa kwa kuwapa zawadi ya pesa famila tatu za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: