Mradi wa upanuzi wa haram tukufu upande wa upauaji wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).. sababu zake.. malengo na falsafa ya usanifu wake..

Maoni katika picha
Kwa nini umefanyika mradi huu?

Toka mwaka (2007 m) viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu walikua na fikra ya kupanua haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani jengo lililo kuwepo lilikua haliwezi kubeba idadi kubwa ya mazuwaru (watu wanakuja kufanya ziara) watukufu hasa katika ziara maalumu za milionea (zinazo fanywa na mamilioni ya watu).

Pia idadi ya mazuwaru imekua ikiongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuwa wazi ataba hizi kwa watu wote duniani, toka ulipo rejea uongozi wa kisheria wa ataba hizo chini ya Marjaa dini mkuu, baada ya kuanguka utawala uliopita (wa Sadam) (09/04/2003 m) utawala ambao haukuijali Iraq na Ataba zake, tena Ataba zilipuuzwa zaidi kwa miaka mingi na akawa anazitumia kwa maslahi yake namna atakavyo.

Jambo hilolilipelekea kuwa na umuhimu wa kukarabati jengo la zamani kwa kulipanua na kulipaua, upanuzi wa aina hii ndio wa kwanza kufanywa tangu kufunguliwa rasmi kwa jengo hili mwaka wa 690 h, upanuzi huu umezingatia mambo yatuatayo:

  • 1- Kuto tofautiana mapambo mapya na yale ya zamani, yaliyo jengwa kwa kufata fani za kiiraq za zamani zilizo kua katika karne ya pili hadi ya saba hijiriyya, ambayo yanahusisha Maqranaswat Bagdadiyya na yaliyo ongezwa hivi sasa miongoni mwa fani za kiiraq za kiasili kama vile kuweka Kashi Karbalai na Maraya za Fasifsaaiyya.
  • 2- Kuto guswa jengo la haram la asili, halikubomolewa wala kubadilishwa.
  • 3- Kuendelea kuingiza idadi kubwa ya mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) kila siku, na kuwafanya wahisi kua wapo ndani ya haram na sio ndani ya uwanja wa haram (sahani) kupitia muonekano wa jengo na huduma zinazo tolewa.
  • 4- Kuingiza idadi kubwa zaidi ya mazuwaru hasa katika ziara za milionea ambazo huhudhuriwa na watu wengi zaidi kila mwaka.
  • 5- Kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mazuwari ili waweze kutekeleza ibada zao kwa utulivu, wasisumbuliwe na mabadiriko ya hali ya hewa, kama vile baridi kali wakati wa baridi au joto kali msimu wa joto.
  • 6- Kuweka uwiano baina ya mazingira ya sasa na ya zamani, na kubakisha hali iliyo kuwepo zamani ambayo mtu anapo ingia ndani ya haram anaendelea kuona minara ya haram japo kidogo.
  • 7- Kujengwa paa jipya katika sehemu ya uwanja wa haramu iliyo kua wazi pamoja na kuimarisha nguzo za zamani katika mradi wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuweka zege imara, baada ya kukamilika kwa miradi hii miwili litaonekana jengo moja imara zaidi katika sekta zote za jengo kama vile:

  1. Haram yake ya zamani.
  2. Uanja wake wa zamani ambao umeezekwa na kubakia unafanana na wazamani kidogo.
  3. Uzio wake wa zamani.
  4. Upanuzi wake mpya katika nguzo zake za uzio.

Uwanja mpya wa haram tukufu ulio ezekwa ndio mbadala wa uwanja wa zamani ulio kua wazi, utahusisha eneo lote linalo zunguka Ataba tukufu na utakua uwanja mmoja, kutokana na miradi ya baadae itakayo endelea, pale zitakapo patikana pesa za kulipa fidia watu wanao zunguka eneo la Ataba, pamoja na pesa za ujenzi wa mradi huo.

  • 8- Falsafa ya usanifu wa hapa iwe na uhusiano wa kiroho kutokana na unyeti wa eneo hili tukufu.

Falsafa ya usanifu

Ili kuhakikisha usanifu wa jengo hili unaendana na hadhi ya mwenye malalo haya matukufu (a.s) usanifu wa jengo hili ulizingatia mambo yafuatayo:

  1. Usanifu wa uwezekaji wa paa ya vioo kuna ashiria mambo mawili:

  • - Kuna ashiria mahema aliyo kua akiyasimamia na kuyalinda Abulfadhil Abbasi (a.s)
  • - Kuna ashiria idadi ya miaka ya umri wake mtukufu.

  1. Usanifu wa nguzo 4 kubwa, kila nguzo iliyo kuwepo katika uwanja wa zamani juu yake kuna kubba nne kubwa, kubba moja ina ashiria bibi Zainabu (a.s) na tatu zina ashiria ndugu watatu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walio uawa pamoja naye katika vita vya Twafu na wakazikwa pamoja na ndugu yao imamu Hussein (a.s) nao ni: (Abdallah, Jafari na Othman –a.s-).
  2. Usanifu wa kubba ndogo (14), kubba ya kwanza ina ashiria mtume (s.a.w.w) na ya pili bibi Fatuma (a.s) na 12 kila moja ina ashiria imamu miongoni mwa maimamu kumi na mbili wa nyumba ya mtume (s.a.w.w) nao ndio makhalifa wake alio wateua, wa kwanza wao ni Amirul Mu-uminina (a.s) na wa mwisho wao ni Hujjat bun Hassan (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: