Kamati ya maandalizi ikaendelea kusema kua: “Kuna kamati ya wataalamu imeundwa na wanachuoni wa hauza na wasomi wa kisekula, watakao chuja mada zitakazo wasilishwa katika viwango vya kielimu kwa kufuata kanuni zinazo tambulika, ili kongamano liendane na malengo yake na uwe msingi imara wa muendelezo wa makongamano mengine yenye manufaa zaidi katika hauza ya Najafu, mialiko ilitolewa kwa wasomi wa hauza na wa kisekula ili waweze kushiriki, mada zitakazo tolewa ni:
Sehemu ya kwanza: Makhatibu wa Husseiniyya
- Maendeleo ya kihistoria katika mimbari ya Husseiniyya.
- Vigezo vya kielimu kwa khatibu (mzungumzaji).
- Changamito za sasa zinazo shambulia mimbari ya Husseiniyya.
- Vitisho vya kielimu katika mada zinazo wasilishwa.
- Sifa za pekee katika hotuba za Husseiniyya.
- Umuhimu wa mimbari za Husseiniyya katika jamii na dini.
- Athari zilizopo katika kuainisha madhumuni ya hotuba.
- Nafasi ya mimbari ya Husseiniyya katika kudumisha uislamu.
- Mimbari ya Husseiniyya kati ya uasili na uhuishwaji wake.
Sehemu ya pili: Utajiri wa swala la Husseiniyya
- Nafasi ya utajiri wa swala la Husseiniyya.
- Nafasi ya utajiri katika kusisitizia upande wa kimaumbile.
- Kutofautiana malengo ya utajiri kutokana na kutofautiana kwa hali za jamii.
- Adabu katika swala la Husseiniyya.
- Maendeleo yake katika hisia za watu.
- Visa na matukio vinapingana au vinaoana.
Sehemu ya tatu: Makhatibu na washairi katika swala la Hussein.
- Shekh Muhammad Ali Ya’aqubiy
- Sayyid Swaleh Hilliy
- Sayyid Jawaad Shibri
- Shekh Ahmad Waailiy
- Sayyid Ridha Hindiy
- Shekh Abdul-muni’imu Fartusi
Kumbuka kua kongamano hili, lina umuhimu mkubwa wa kusambaza tamaduni za Ahlulbait (a.s) na kueneza maana ya uislamu mtukufu katika jamii inayo kubwa na vikwazo kutoka kila upande, kifikra, kiteknelojia, katika mitandao ya kijamii, na uharaka wa kusafirisha habari uliopo hivi sasa bila vikwazo vyovyote.. jambo ambalo limeonyesha umuhimu mkubwa kwa wazungumzaji wa mimbari ya Husseiniyya wenye aina zote za utukufu, uadilifu na roho ya kuvumiliana, na kuachana na kila aina ya ubaguzi na chuki zinazo pelekea uhasama, kupigana na kutengana baina wa waislamu, wazungumzaji wa mimbari ya Husseiniyya waenzi utamaduni wao wa kuhakikisha waislamu wanaishi kwa amani na watu wote.